Jeremiah 50:39 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kwa hiyo wanyama wa porini, mbwamwitu pamoja na mbuni, watakaa Babuloni. Hapatakaliwa kamwe na watu vizazi vyote vijavyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo, viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo, nao bundi watakaa humo. Kamwe haitakaliwa tena wala watu hawataishi humo kizazi hadi kizazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, wanyama wakali wa jangwani, pamoja na mbwa-mwitu, watakaa huko, na mbuni watakaa ndani yake; wala haitakaliwa na watu milele; wala hapana mtu atakayekaa huko tangu kizazi hata kizazi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kwa hiyo wanyama wa porini, mbwamwitu pamoja na mbuni, watakaa Babuloni. Hapatakaliwa kamwe na watu vizazi vyote vijavyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hivyo viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo, nao bundi watakaa humo. Kamwe haitakaliwa tena wala watu hawataishi humo kutoka kizazi hadi kizazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo, viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo, nao bundi watakaa humo. Kamwe haitakaliwa tena wala watu hawataishi humo kutoka kizazi hadi kizazi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, wanyama wakali wa jangwani, pamoja na mbwamwitu, watakaa huko, na mbuni watakaa ndani yake; wala haitakaliwa na watu milele; wala hakuna mtu atakayekaa huko tangu kizazi hadi kizazi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kwa hiyo wanyama wa porini, mbwamwitu pamoja na mbuni, watakaa Babuloni. Hapatakaliwa kamwe na watu vizazi vyote vijavyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo watakaa humo nyama wa porini na mbwa wa mwitu, nao mbuni watakaa mwake, lakini watu hawatakaa humo kale na kale, ila utakaa pasipo mtu kwa vizazi na vizazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, wanyama wakali wa jangwani, pamoja na mbwa-mwitu, watakaa huko, na mbuni watakaa ndani yake; wala haitakaliwa na watu milele; wala hapana mtu atakayekaa huko tangu kizazi hata kizazi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo nyama wa pori, imbwa wa pori pamoja na mbuni, watakaa Babeli. Hakutakaliwa hata kidogo na watu wa vizazi vyote vinavyokuja.