Jeremiah 50:42 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wameshika pinde zao na mikuki; ni watu wakatili na wasio na huruma. Vishindo vyao ni kama mvumo wa bahari, wamepanda farasi. Wamejipanga tayari kwa vita, dhidi yako wewe Babuloni!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wamejifunga pinde na mikuki; ni wakatili na hawana huruma. Wanatoa sauti kama bahari inayounguruma wanapoendesha farasi wao; wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita ili kukushambulia, ee Binti Babeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wanashika upinde na mkuki; Ni wakatili, hawana huruma; Sauti yao inanguruma kama bahari, Nao wamepanda farasi; Kila mmoja amejipanga kama aendaye vitani, Juu yako, Ee binti Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wameshika pinde zao na mikuki; ni watu wakatili na wasio na huruma. Vishindo vyao ni kama mvumo wa bahari, wamepanda farasi. Wamejipanga tayari kwa vita, dhidi yako wewe Babuloni!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wamejifunga pinde na mikuki; ni wakatili na wasio na huruma. Wanasikika kama bahari inayonguruma wanapoendesha farasi zao; wanakuja kama watu waliojipanga kwa vita ili kukushambulia, Ee Binti Babeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wamejifunga pinde na mikuki; ni wakatili na wasio na huruma. Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma wanapoendesha farasi zao; wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita ili kukushambulia, ee Binti Babeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wanashika upinde na mkuki; Ni wakatili, hawana huruma; Sauti yao inanguruma kama bahari, Nao wamepanda farasi; Kila mmoja amejipanga kama aendaye vitani, Juu yako, Ee binti Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wameshika pinde zao na mikuki; ni watu wakatili na wasio na huruma. Vishindo vyao ni kama mvumo wa bahari, wamepanda farasi. Wamejipanga tayari kwa vita, dhidi yako wewe Babuloni!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wanashika pindi na mikuki, ni wakorofi, hawana huruma, sauti zao huvuma kama bahari, hupanda farasi, wako tayari kupiga kama mtu wa vitani; wanakujia wewe, binti Babeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wanashika upinde na mkuki; Ni wakatili, hawana huruma; Sauti yao inanguruma kama bahari, Nao wamepanda farasi; Kila mmoja amejipanga kama aendaye vitani, Juu yako, Ee binti Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wameshika pinde zao na mikuki; ni watu wakali wasiokuwa na huruma. Vishindo vyao ni kama uvumi wa bahari, wamepanda juu ya farasi. Wamejipanga tayari kwa vita na wewe Babeli!