Jeremiah 50:43 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme wa Babuloni amesikia habari zao, nayo mikono yake ikawa kama kamba. Ameshikwa na dhiki na uchungu kama mama anayejifungua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu, nayo mikono yake imelegea. Uchungu umemshika, maumivu kama ya mwanamke katika uchungu wa kuzaa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme wa Babeli amesikia habari zao, Na mikono yake imekuwa dhaifu; Dhiki imemshika, na maumivu, Kama ya mwanamke katika utungu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme wa Babuloni amesikia habari zao, nayo mikono yake ikawa kama kamba. Ameshikwa na dhiki na uchungu kama mama anayejifungua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu hao, nayo mikono yake imelegea. Uchungu umemshika, maumivu kama yale ya mwanamke aliye katika utungu wa kuzaa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu, nayo mikono yake imelegea. Uchungu umemshika, maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme wa Babeli amesikia habari zao, Na mikono yake imekuwa dhaifu; Dhiki imemshika, na maumivu, Kama ya mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme wa Babuloni amesikia habari zao, nayo mikono yake ikawa kama kamba. Ameshikwa na dhiki na uchungu kama mama anayejifungua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme wa Babeli amezisikia habari zao; ndipo, mikono yake ilipolegea, masongano yakamshika na uchungu, kama mwanamke anayetaka kuzaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme wa Babeli amesikia habari zao, Na mikono yake imekuwa dhaifu; Dhiki imemshika, na maumivu, Kama ya mwanamke katika utungu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme wa Babeli amesikia habari zao. Kwa hiyo, mikono yake ikaregea. Ameshikwa na huzuni na uchungu, kama mama anayezaa.