Jeremiah 50:45 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, sikilizeni mpango ambao mimi Mwenyezi-Mungu nimepanga dhidi ya Babuloni pamoja na mambo niliyokusudia kuitendea nchi ya Wakaldayo: Hakika watoto wao wataburutwa na kuchukuliwa; kweli kutakuwa na mshangao mkubwa katika makao yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, sikia ambacho Mwenyezi Mungu amepanga dhidi ya Babeli, kile alichokusudia dhidi ya nchi ya Wakaldayo: Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali. Yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, lisikieni shauri la Bwana, Alilolifanya juu ya Babeli; Na makusudi yake aliyoyakusudia Juu ya nchi ya Wakaldayo. Hakika watawaburura, naam, wadogo wa kundi; Hakika malisho yao yatafadhaika kwa ajili yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, sikilizeni mpango ambao mimi Mwenyezi-Mungu nimepanga dhidi ya Babuloni pamoja na mambo niliyokusudia kuitendea nchi ya Wakaldayo: Hakika watoto wao wataburutwa na kuchukuliwa; kweli kutakuwa na mshangao mkubwa katika makao yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, sikia kile BWANA alichokipanga dhidi ya Babeli, kile alichokusudia dhidi ya nchi ya Wakaldayo: Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali, ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, sikia kile bwana alichokipanga dhidi ya Babeli, kile alichokusudia dhidi ya nchi ya Wakaldayo: Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali. Yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, lisikieni shauri la BWANA, Alilolifanya juu ya Babeli; Na makusudi yake aliyoyakusudia Juu ya nchi ya Wakaldayo. Hakika watawaburura, naam, wadogo wa kundi; Hakika malisho yao yatafadhaika kwa ajili yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, sikilizeni mpango ambao mimi Mwenyezi-Mungu nimepanga dhidi ya Babuloni pamoja na mambo niliyokusudia kuitendea nchi ya Wakaldayo: Hakika watoto wao wataburutwa na kuchukuliwa; kweli kutakuwa na mshangao mkubwa katika makao yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo lisikieni shauri la Bwana, aliloukatia Babeli, nayo mawazo yake, aliyoiwazia nchi ya Wakasidi kwamba: kweli watakaowakokotakokota ndio wadogo wa makundi, kweli nchi yao yenyewe itawastukia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, lisikieni shauri la BWANA, Alilolifanya juu ya Babeli; Na makusudi yake aliyoyakusudia Juu ya nchi ya Wakaldayo. Hakika watawaburura, naam, wadogo wa kundi; Hakika malisho yao yatafadhaika kwa ajili yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, musikilize mupango ambao Yawe amepanga juu ya Babeli pamoja na mambo aliyokusudia kuifanyia inchi ya Wakaldea: Hakika, watoto wao wadogo watakokotwa na kukamatwa; kweli kutakuwa mushangao mukubwa katika makao yao!