Jeremiah 50:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watauliza njia ya kwenda Siyoni, huku nyuso zao zimeelekea huko, wakisema, ‘Njoni!’ Nao watajiunga na Mwenyezi-Mungu katika agano la milele ambalo kamwe halitasahauliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wataulizia njia iendayo Sayuni na kuelekeza nyuso zao huko. Watakuja na kuambatana na Mwenyezi Mungu katika agano la milele ambalo halitasahaulika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watauliza habari za Sayuni, na nyuso zao zitaelekea huko, wakisema, Njoni ninyi, mjiunge na Bwana, kwa agano la milele ambalo halitasahauliwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watauliza njia ya kwenda Siyoni, huku nyuso zao zimeelekea huko, wakisema, ‘Njoni!’ Nao watajiunga na Mwenyezi-Mungu katika agano la milele ambalo kamwe halitasahauliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wataiuliza njia iendayo Sayuni na kuelekeza nyuso zao huko. Watakuja na kuambatana na BWANA katika Agano la milele ambalo halitasahaulika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wataiuliza njia iendayo Sayuni na kuelekeza nyuso zao huko. Watakuja na kuambatana na bwana katika agano la milele ambalo halitasahaulika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watauliza njia ya kwenda Sayuni, na nyuso zao zitaelekea huko, wakisema, Njooni ninyi, mjiunge na BWANA, kwa agano la milele ambalo halitasahauliwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watauliza njia ya kwenda Siyoni, huku nyuso zao zimeelekea huko, wakisema, ‘Njoni!’ Nao watajiunga na Mwenyezi-Mungu katika agano la milele ambalo kamwe halitasahauliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watauliza njia ya kwenda Sioni; ndiko, nyuso zao zinakoelekea kwamba: Njoni kuandamana na Bwana, tukifanya agano la kale na kale lisilosahauliwa tena!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watauliza habari za Sayuni, na nyuso zao zitaelekea huko, wakisema, Njoni ninyi, mjiunge na BWANA, kwa agano la milele ambalo halitasahauliwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watauliza njia ya kwenda Sayuni, na nyuso zao zikielekea huko, wakisema: Mukuje! Nao watajiunga na Yawe katika agano la milele ambalo halitasahauliwa hata kidogo.