Jeremiah 50:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Watu wangu walikuwa kondoo waliopotea; wachungaji wao wamewapotosha, wakawageuza kuelekea milimani; walitembea toka mlima hadi kilima, wakasahau zizi lao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea; wachungaji wao wamewapotosha na kuwafanya wazurure mlimani. Walitangatanga juu ya mlima na kilima, na kusahau mahali pao pa kupumzikia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Watu wangu walikuwa kondoo waliopotea; wachungaji wao wamewapotosha, wakawageuza kuelekea milimani; walitembea toka mlima hadi kilima, wakasahau zizi lao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea; wachungaji wao wamewapotosha na kuwasababisha kuzungukazunguka juu ya milima. Walitangatanga juu ya mlima na kilima na kusahau mahali pao wenyewe pa kupumzikia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea; wachungaji wao wamewapotosha na kuwasababisha kuzurura juu ya milima. Walitangatanga juu ya mlima na kilima, na kusahau mahali pao wenyewe pa kupumzikia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hadi kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Watu wangu walikuwa kondoo waliopotea; wachungaji wao wamewapotosha, wakawageuza kuelekea milimani; walitembea toka mlima hadi kilima, wakasahau zizi lao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walio ukoo wangu walikuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao waliwapoteza, wakatangatanga milimani, walipotoka mlimani wakaendea kilima kingine, wakakisahau kituo chao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wangu walikuwa kama kondoo waliopotea; wachungaji wao wamewapotosha, wakawageuza kuelekea kwenye milima; walitembea toka mulima mpaka kilima, wakasahau makao yao.