Jeremiah 50:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, mimi nitachochea mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini washambulie Babuloni. Watajiandaa kuishambulia Babuloni na kuiteka. Mishale yao ni kama shujaa hodari asiyerudi mikono mitupu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babeli muungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini. Watashika nafasi zao dhidi yake, naye kutokea kaskazini atatekwa. Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari, ambao hawawezi kurudi mikono mitupu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana juu ya Babeli nitaamsha na kuleta kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini; nao watajipanga juu yake; kutoka huko atatwaliwa; mishale yao itakuwa kama ya mtu shujaa aliye stadi; hapana hata mmoja utakaorudi bure.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, mimi nitachochea mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini washambulie Babuloni. Watajiandaa kuishambulia Babuloni na kuiteka. Mishale yao ni kama shujaa hodari asiyerudi mikono mitupu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babeli muungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini. Watashika nafasi zao dhidi yake, naye kwa kutokea kaskazini atatekwa. Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari ambao hawawezi kurudi mikono mitupu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babeli muungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini. Watashika nafasi zao dhidi yake, naye kutokea kaskazini atatekwa. Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari, ambao hawawezi kurudi mikono mitupu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana juu ya Babeli nitaamsha na kuleta kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini; nao watajipanga juu yake; kutoka huko atatwaliwa; mishale yao itakuwa kama ya mtu shujaa aliye stadi; hakuna hata mmoja utakaorudi bure.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, mimi nitachochea mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini washambulie Babuloni. Watajiandaa kuishambulia Babuloni na kuiteka. Mishale yao ni kama shujaa hodari asiyerudi mikono mitupu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mtaniona mimi, nikiinua mkutano wa mataifa makubwa yatokayo upande wa kaskazinni, niyapandishe kwenda Babeli; watakapojipanga, hapohapo ndipo, utakapotekwa. Mishale yao ni kama ya mpiga vita mwerevu asiyerudi mikono mitupu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana juu ya Babeli nitaamsha na kuleta kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini; nao watajipanga juu yake; kutoka huko atatwaliwa; mishale yao itakuwa kama ya mtu shujaa aliye stadi; hapana hata mmoja utakaorudi bure.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana, mimi nitachochea mataifa makubwa kutoka inchi ya kaskazini washambulie inchi ya Babeli. Watajitayarisha kuishambulia inchi ya Babeli na kuiteka. Mishale yao ni kama shujaa hodari asiyerudi mikono mitupu.