Jeremiah 51:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu amezichochea roho za wafalme wa Media, kwa maana amenuia kuiangamiza Babuloni. Naam, hicho ndicho kisasi cha Mwenyezi-Mungu; analipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake. Noeni mishale yenu! Chukueni ngao!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Noeni mishale, chukueni ngao! Mwenyezi Mungu amewaamsha wafalme wa Wamedi, kwa sababu nia yake ni kuangamiza Babeli. Mwenyezi Mungu atalipiza kisasi, kisasi kwa ajili ya Hekalu lake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Inoeni hiyo mishale; zishikeni ngao kwa nguvu; Bwana ameziamsha roho za wafalme wa Wamedi; kwa sababu shauri lake ni juu ya Babeli auangamize; maana ni kisasi cha Bwana, kisasi cha hekalu lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu amezichochea roho za wafalme wa Media, kwa maana amenuia kuiangamiza Babuloni. Naam, hicho ndicho kisasi cha Mwenyezi-Mungu; analipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake. Noeni mishale yenu! chukueni ngao!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Noeni mishale, chukueni ngao! BWANA amewaamsha wafalme wa Wamedi, kwa sababu nia yake ni kuangamiza Babeli. BWANA atalipiza kisasi, kisasi kwa ajili ya Hekalu lake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Noeni mishale, chukueni ngao! bwana amewaamsha wafalme wa Wamedi, kwa sababu nia yake ni kuangamiza Babeli. bwana atalipiza kisasi, kisasi kwa ajili ya Hekalu lake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Inoeni hiyo mishale; zishikeni ngao kwa nguvu; BWANA ameziamsha roho za wafalme wa Wamedi; kwa sababu shauri lake ni juu ya Babeli auangamize; maana ni kisasi cha BWANA, kisasi cha hekalu lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu amezichochea roho za wafalme wa Media, kwa maana amenuia kuiangamiza Babuloni. Naam, hicho ndicho kisasi cha Mwenyezi-Mungu; analipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake. Noeni mishale yenu! Chukueni ngao!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Inoeni mishale! Zishikeni ngao! Bwana ameziinua roho za wafalme wa Wamedi, kwani mawazo yake yameuelekea Babeli, auangamize, kwani hili ndilo lipizi lake Bwana, alilipizie Jumba lake takatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Inoeni hiyo mishale; zishikeni ngao kwa nguvu; BWANA ameziamsha roho za wafalme wa Wamedi; kwa sababu shauri lake ni juu ya Babeli auangamize; maana ni kisasi cha BWANA, kisasi cha hekalu lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe amezichochea roho za wafalme wa Wamedi, kwa maana amekusudia kuiangamiza Babeli. Kweli, hicho ndicho kisasi cha Yawe; analipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake. Munoe mishale yenu! Mutwae ngao!