Jeremiah 51:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Twekeni bendera ya vita kushambulia kuta za Babuloni. Imarisheni ulinzi; wekeni walinzi; tayarisheni mashambulizi. Mwenyezi-Mungu amepanga na kutekeleza mambo aliyosema juu ya wakazi wa Babuloni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Inueni bendera dhidi ya kuta za Babeli! Imarisheni ulinzi, wekeni walinzi, andaeni waviziaji! Mwenyezi Mungu atatimiza kusudi lake, amri yake juu ya watu wa Babeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Twekeni bendera juu ya kuta za Babeli, yatieni malindo nguvu, wawekeni walinzi, tengenezeni waviziao; kwa maana Bwana ameazimia na kutenda yote aliyoyasema juu yao wakaao Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Twekeni bendera ya vita kushambulia kuta za Babuloni. Imarisheni ulinzi; wekeni walinzi; tayarisheni mashambulizi. Mwenyezi-Mungu amepanga na kutekeleza mambo aliyosema juu ya wakazi wa Babuloni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Twekeni bendera juu ya kuta za Babeli! Imarisheni ulinzi, wekeni walinzi, andaeni waviziao! BWANA atatimiza kusudi lake, amri yake juu ya watu wa Babeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Twekeni bendera juu ya kuta za Babeli! Imarisheni ulinzi, wekeni walinzi, andaeni waviziao! bwana atatimiza kusudi lake, amri yake juu ya watu wa Babeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Twekeni bendera ya vita juu ya kuta za Babeli, imarisheni ulinzi, wawekeni walinzi, tayarisheni waviziao; kwa maana BWANA ameazimia na kutenda yote aliyoyasema juu yao wakaao Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Twekeni bendera ya vita kushambulia kuta za Babuloni. Imarisheni ulinzi; wekeni walinzi; tayarisheni mashambulizi. Mwenyezi-Mungu amepanga na kutekeleza mambo aliyosema juu ya wakazi wa Babuloni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Twekeni bendera zielekeazo kuta za Babeli! Malindo yatieni nguvu mkiongeza walinzi na kuweka nao wenye kuvizia! Kwani Bwana aliyoyawaza huyafanya, ayatimize nayo yale, aliyoyasema, ya kuwa atawafanyizia wakaao Babeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Twekeni bendera juu ya kuta za Babeli, yatieni malindo nguvu, wawekeni walinzi, tengenezeni waviziao; kwa maana BWANA ameazimia na kutenda yote aliyoyasema juu yao wakaao Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mupandishe bendera ya vita kwa kushambulia kuta za Babeli. Muimarishe walinzi, muweke walinzi, mutayarishe mashambulizi. Yawe amepanga na kutimiza mambo aliyosema juu ya wakaaji wa Babeli.