Jeremiah 51:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mtu ni mpumbavu bila maarifa, kila mhunzi anaaibishwa na vinyago vyake; maana sanamu zake ni udanganyifu mtupu, wala hazina pumzi ndani yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kila mtu ni mjinga na hana maarifa; kila sonara ameaibishwa na sanamu zake. Vinyago vyake ni vya udanganyifu; havina pumzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mtu ni mpumbavu bila maarifa, kila mhunzi anaaibishwa na vinyago vyake; maana sanamu zake ni udanganyifu mtupu, wala hazina pumzi ndani yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kila mtu hana ufahamu na hana maarifa; kila sonara ameaibika kwa sanamu zake. Vinyago vyake ni vya udanganyifu, havina pumzi ndani yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kila mtu ni mjinga na hana maarifa; kila sonara ameaibishwa na sanamu zake. Vinyago vyake ni vya udanganyifu, havina pumzi ndani yavyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mtu ni mpumbavu bila maarifa, kila mhunzi anaaibishwa na vinyago vyake; maana sanamu zake ni udanganyifu mtupu, wala hazina pumzi ndani yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, kila mtu anapopumbaa tu, asijue yatokako, hata kila mfua dhahabu hupatwa na soni kwa ajili ya kinyago chake, kwani alichokitengeneza ni uwongo tu, hata pumzi haimo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mutu ni mupumbafu bila maarifa, kila mufua vyuma anapatishwa haya na miungu yake; maana sanamu zake ni udanganyifu mutupu, wala hazina pumzi ndani yake.