Jeremiah 51:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi ninapingana nawe ewe mlima mharibifu, mlima unaoharibu dunia nzima! Nasema mimi Mwenyezi-Mungu. Nitanyosha mkono wangu dhidi yako, nitakuangusha kutoka miambani juu na kukufanya kuwa mlima uliochomwa moto;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mimi niko kinyume nawe, ee mlima unaoharibu, wewe uangamizaye dunia yote,” asema Mwenyezi Mungu. “Nitanyoosha mkono wangu dhidi yako, nikuvingirishe kutoka kilele cha mwamba, na kukufanya mlima ulioteketezwa kwa moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, mimi ni juu yako, Ee mlima uharibuo, asema Bwana; wewe uiharibuye dunia nzima; nami nitaunyosha mkono wangu juu yako, na kukufingirisha chini toka majabalini; nami nitakufanya kuwa mlima ulioteketezwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi ninapingana nawe ewe mlima mharibifu, mlima unaoharibu dunia nzima! Nasema mimi Mwenyezi-Mungu. Nitanyosha mkono wangu dhidi yako, nitakuangusha kutoka miambani juu na kukufanya kuwa mlima uliochomwa moto;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mimi niko kinyume nawe, Ee mlima unaoharibu, wewe uangamizaye dunia yote,” asema BWANA. “Nitanyosha mkono wangu dhidi yako, nikuvingirishe kutoka kwenye kilele cha mwamba, na kukufanya mlima ulioteketezwa kwa moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mimi niko kinyume nawe, ee mlima unaoharibu, wewe uangamizaye dunia yote,” asema bwana. “Nitanyoosha mkono wangu dhidi yako, nikuvingirishe kutoka kwenye kilele cha mwamba, na kukufanya mlima ulioteketezwa kwa moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, mimi niko juu yako, Ee mlima uharibuo, asema BWANA; wewe uiharibuye dunia nzima; nami nitaunyosha mkono wangu juu yako, na kukubingirisha chini toka majabalini; nami nitakufanya kuwa mlima ulioteketezwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi ninapingana nawe ewe mlima mharibifu, mlima unaoharibu dunia nzima! Nasema mimi Mwenyezi-Mungu. Nitanyosha mkono wangu dhidi yako, nitakuangusha kutoka miambani juu na kukufanya kuwa mlima uliochomwa moto;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Utaniona, nikikujia wewe, mlima uangamizao! Umeziangamiza nchi zote, lakini nimekukunjulia mkono wangu, nikuporomoshe, utoke miambani; nitakugeuza kuwa mlima uliochomwa moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, mimi ni juu yako, Ee mlima uharibuo, asema BWANA; wewe uiharibuye dunia nzima; nami nitaunyosha mkono wangu juu yako, na kukufingirisha chini toka majabalini; nami nitakufanya kuwa mlima ulioteketezwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi ninapingana nawe, ewe mulima muharibifu, mulima unaoharibu dunia nzima! –Ni ujumbe wa Yawe.– Nitanyoosha mukono wangu juu yako kwa kukuazibu, nitakuangusha kutoka juu kwenye mawe makubwa na kukufanya kuwa mulima uliochomwa kwa moto.