Jeremiah 51:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema hivi: “Babuloni ni kama uwanja wa kupuria nafaka wakati unapotayarishwa. Lakini bado kidogo tu, wakati wa mavuno utaufikia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: “Binti Babeli ni kama sakafu ya kupuria wakati inapokanyagwa; wakati wa kumvuna utakuja upesi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi; Binti Babeli amekuwa kama sakafu ya kufikichia wakati wa kukanyagwa kwake; bado kitambo kidogo na wakati wa mavuno utafika kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema hivi: “Babuloni ni kama uwanja wa kupuria nafaka wakati unapotayarishwa. Lakini bado kidogo tu, wakati wa mavuno utaufikia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Binti Babeli ni kama sakafu ya kupuria wakati inapokanyagwa; wakati wa kumvuna utakuja upesi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Binti Babeli ni kama sakafu ya kupuria wakati inapokanyagwa; wakati wa kumvuna utakuja upesi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi; Binti Babeli amekuwa kama sakafu ya kufikichia wakati wa kukanyagwa kwake; bado kitambo kidogo na wakati wa mavuno utafika kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema hivi: “Babuloni ni kama uwanja wa kupuria nafaka wakati unapotayarishwa. Lakini bado kidogo tu, wakati wa mavuno utaufikia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Binti Babeli anafanana na mahali pa kupigia ngano pakitengenezwa na kupondwa, siku za mavuno zitaujia bado kidogo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi; Binti Babeli amekuwa kama sakafu ya kufikichia wakati wa kukanyagwa kwake; bado kitambo kidogo na wakati wa mavuno utafika kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Babeli ni kama uwanja wa kupepetea ngano wakati unapotayarishwa. Lakini bado kidogo tu, wakati wa mavuno utaufikia.