Jeremiah 51:35 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Yerusalemu na waseme: “Babuloni na ulipizwe ukatili uleule, tuliotendwa sisi pamoja na jamaa zetu! Babuloni ipatilizwe kwa umwagaji wa damu yetu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jeuri iliyotendewa miili yetu na iwe juu ya Babeli,” ndivyo wasemavyo wakaaji wa Sayuni. “Damu yetu na iwe juu ya wakaaji wa Babeli,” asema Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Udhalimu niliotendwa mimi, na uliotendwa mwili wangu, umpate Babeli; ndivyo atakavyosema yeye akaaye Sayuni; na Yerusalemu atasema, Damu yangu na iwe juu yao wakaao katika Ukaldayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Yerusalemu na waseme: “Babuloni na ulipizwe ukatili uleule, tuliotendwa sisi pamoja na jamaa zetu! Babuloni ipatilizwe kwa umwagaji wa damu yetu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jeuri iliyofanyiwa miili yetu na iwe juu ya Babeli,” ndivyo wasemavyo wakaao Sayuni. “Damu yetu na iwe juu ya wale waishio Babeli,” asema Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jeuri iliyofanyiwa miili yetu na iwe juu ya Babeli,” ndivyo wasemavyo wakaao Sayuni. “Damu yetu na iwe juu ya wale waishio Babeli,” asema Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Udhalimu niliotendwa mimi, na uliotendwa mwili wangu, umpate Babeli; ndivyo atakavyosema yeye akaaye Sayuni; na Yerusalemu atasema, Damu yangu na iwe juu yao wakaao katika Ukaldayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Yerusalemu na waseme: “Babuloni na ulipizwe ukatili uleule, tuliotendwa sisi pamoja na jamaa zetu! Babuloni ipatilizwe kwa umwagaji wa damu yetu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Makorofi, waliyonitendea, nayo miili ya watu, waliowaua kwetu, na iujie Babeli! ndivyo, watakavyosema wakaao Sioni; damu, walizozimwaga kwetu, na ziwajie wakaao katika nchi ya Wakasidi! ndivyo, watakavyosema Wayerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Udhalimu niliotendwa mimi, na uliotendwa mwili wangu, umpate Babeli; ndivyo atakavyosema yeye akaaye Sayuni; na Yerusalemu atasema, Damu yangu na iwe juu yao wakaao katika Ukaldayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Sayuni watasema: Babeli ulipizwe mateso makali yaleyale tuliyotendewa sisi pamoja na jamaa zetu! Yerusalema itasema: Damu yangu ikuwe juu ya wakaaji wa Kaledea.