Jeremiah 51:36 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo asema hivi Mwenyezi-Mungu: “Nitawatetea kuhusu kisa chenu, na kulipiza kisasi kwa ajili yenu. Nitaikausha bahari ya Babuloni na kuvifanya visima vyake vikauke.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Tazama, nitakutetea na kukulipizia kisasi; nitaikausha bahari yake na kuzikausha chemchemi zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, Bwana asema hivi, Tazama, nitakutetea, nami nitatwaa kisasi kwa ajili yako; nami nitaikausha bahari yake, nitaifanya chemchemi yake kuwa pakavu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo asema hivi Mwenyezi-Mungu: “Nitawatetea kuhusu kisa chenu, na kulipiza kisasi kwa ajili yenu. Nitaikausha bahari ya Babuloni na kuvifanya visima vyake vikauke.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, hili ndilo BWANA asemalo: “Tazama, nitatetea shauri lako na kulipiza kisasi kwa ajili yako; nitaikausha bahari yake na kuzikausha chemchemi zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, hili ndilo bwana asemalo: “Tazama, nitatetea shauri lako na kulipiza kisasi kwa ajili yako; nitaikausha bahari yake na kuzikausha chemchemi zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitakutetea, nami nitatwaa kisasi kwa ajili yako; nami nitaikausha bahari yake, nitaifanya chemchemi yake kuwa pakavu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo asema hivi Mwenyezi-Mungu: “Nitawatetea kuhusu kisa chenu, na kulipiza kisasi kwa ajili yenu. Nitaikausha bahari ya Babuloni na kuvifanya visima vyake vikauke.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa hiyo mtaniona, nikiwagombea magomvi yenu, nikiwalipizia malipizi yenu; nitaukausha mto wao mkubwa, navyo visima vyao nitavinyima maji, vipwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitakutetea, nami nitatwaa kisasi kwa ajili yako; nami nitaikausha bahari yake, nitaifanya chemchemi yake kuwa pakavu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo Yawe anasema hivi: Nitawatetea juu ya maneno yenu, na kulipiza kisasi kwa ajili yenu. Nitaikausha bahari ya Babeli na kuvifanya visima vyake vikauke.