Jeremiah 51:39 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakiwa na uchu mkubwa nitawaandalia karamu: Nitawalewesha mpaka wapepesuke; nao watalala usingizi wa daima na hawataamka tena. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wakiwa wameamshwa, nitawaandalia karamu na kuwafanya walewe, ili washangilie kwa kicheko, kisha walale milele na wasiamke,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakiingiwa na ukali, nitawafanyizia karamu yao, nami nitawalevya, wapate kufurahi, na kulala usingizi wa milele, wasiamke tena, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakiwa na uchu mkubwa nitawaandalia karamu: nitawalewesha mpaka wapepesuke; nao watalala usingizi wa daima na hawataamka tena. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wakati wakiwa wameamshwa, nitawaandalia karamu na kuwafanya walewe, ili wapige kelele kwa kicheko, kisha walale milele na wasiamke,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wakati wakiwa wameamshwa, nitawaandalia karamu na kuwafanya walewe, ili wapige kelele kwa kicheko, kisha walale milele na wasiamke,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakiingiwa na ukali, nitawafanyia karamu yao, nami nitawalevya, wapate kufurahi, na kulala usingizi wa milele, wasiamke tena, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakiwa na uchu mkubwa nitawaandalia karamu: Nitawalewesha mpaka wapepesuke; nao watalala usingizi wa daima na hawataamka tena. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini vichwa vyao vitakapokuwa vinene, ndipo, nitakapowapa vinywaji vyao vya kuwalevya, wapige vigelegele, kisha walale usingizi wa kale na kale, wasiamke tena; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakiingiwa na ukali, nitawafanyizia karamu yao, nami nitawalevya, wapate kufurahi, na kulala usingizi wa milele, wasiamke tena, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakiwa na hamu kubwa nitawatayarishia karamu: nitawalewesha mpaka wapepesuke; nao watalala usingizi wa siku zote na hawataamuka tena. –Ni ujumbe wa Yawe.–