Jeremiah 51:46 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msife moyo wala msiwe na hofu, kwa sababu ya uvumi mnaosikia nchini. Mwaka huu kuna uvumi huu, mwaka mwingine uvumi mwingine; uvumi wa ukatili katika nchi, mtawala mmoja dhidi ya mtawala mwingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msikate tamaa wala msiogope tetesi zitakaposikika katika nchi; tetesi moja inasikika mwaka huu, nyingine mwaka unaofuata; tetesi juu ya jeuri katika nchi, na ya mtawala dhidi ya mtawala.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala isizimie mioyo yenu, wala msiiogope habari itakayosikiwa katika nchi; maana habari itakuja mwaka mmoja, na baadaye mwaka wa pili habari itakuja, na udhalimu katika nchi, mwenye kutawala akishindana na mwenye kutawala.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msife moyo wala msiwe na hofu, kwa sababu ya uvumi mnaosikia nchini. Mwaka huu kuna uvumi huu, mwaka mwingine uvumi mwingine; uvumi wa ukatili katika nchi, mtawala mmoja dhidi ya mtawala mwingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msikate tamaa wala msiogope tetesi zitakaposikika katika nchi; tetesi moja inasikika mwaka huu, nyingine mwaka unaofuata; tetesi juu ya jeuri katika nchi na ya mtawala dhidi ya mtawala.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msikate tamaa wala msiogope tetesi zitakaposikika katika nchi; tetesi moja inasikika mwaka huu, nyingine mwaka unaofuata; tetesi juu ya jeuri katika nchi, na ya mtawala dhidi ya mtawala.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala isizimie mioyo yenu, wala msiiogope habari itakayosikiwa katika nchi; maana habari itakuja mwaka mmoja, na baadaye mwaka wa pili habari itakuja, na udhalimu katika nchi, mwenye kutawala akishindana na mwenye kutawala.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msife moyo wala msiwe na hofu, kwa sababu ya uvumi mnaosikia nchini. Mwaka huu kuna uvumi huu, mwaka mwingine uvumi mwingine; uvumi wa ukatili katika nchi, mtawala mmoja dhidi ya mtawala mwingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mioyo yenu isizimie kwa woga, mtakapozisikia zile habari zitakazosikilika katika nchi hii, mwaka mmoja ikija habari, mwaka mwingine ikija habari tena, nao ukorofi ukizidi katika nchi hii, kwa kuwa watawala nchi watainukiana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala isizimie mioyo yenu, wala msiiogope habari itakayosikiwa katika nchi; maana habari itakuja mwaka mmoja, na baadaye mwaka wa pili habari itakuja, na udhalimu katika nchi, mwenye kutawala akishindana na mwenye kutawala.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musiregee wala musikuwe na hofu, kwa sababu ya habari munazosikia katika inchi. Mwaka huu kuna habari hii, mwaka mwingine habari ingine; habari ya mateso makali katika inchi, mutawala mumoja anapigana na mutawala mwingine.