Jeremiah 51:48 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mbingu, dunia na vyote vilivyomo vitaimba kwa furaha kuhusu kuanguka kwa Babuloni, waangamizi watakapofika kutoka kaskazini kuushambulia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo mbingu na dunia na vyote vilivyomo vitapiga kelele za shangwe juu ya Babeli, kwa kuwa kutoka kaskazini waangamizi watamshambulia,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo, vitaimba kwa furaha juu ya Babeli; kwa maana watu waangamizao watamjilia kutoka kaskazini, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mbingu, dunia na vyote vilivyomo vitaimba kwa furaha kuhusu kuanguka kwa Babuloni, waangamizi watakapofika kutoka kaskazini kuushambulia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo mbingu na dunia na vyote vilivyomo ndani yake vitapiga kelele za shangwe juu ya Babeli, kwa kuwa kutoka kaskazini waharabu watamshambulia,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo mbingu na dunia na vyote vilivyomo ndani yake vitapiga kelele za shangwe juu ya Babeli, kwa kuwa kutoka kaskazini waharabu watamshambulia,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo, vitaimba kwa furaha juu ya Babeli; kwa maana watu waangamizao watamjia kutoka kaskazini, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha mbingu, dunia na vyote vilivyomo vitaimba kwa furaha kuhusu kuanguka kwa Babuloni, waangamizi watakapofika kutoka kaskazini kuushambulia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mbingu na nchi navyo vyote vilivyomo vitakapouzomea Babeli, kwani toka kaskazini waangamizaji wataujia; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo, vitaimba kwa furaha juu ya Babeli; kwa maana watu waangamizao watamjilia kutoka kaskazini, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mbingu, dunia na vyote vinavyokuwa ndani yao vitaimba kwa furaha juu ya kuanguka kwa Babeli, wakati waangamizaji watakapofika kutoka upande wa kaskazini kuushambulia. –Ni ujumbe wa Yawe.–