Jeremiah 51:50 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nyinyi mlinusurika kifo, ondokeni sasa, wala msisitesite! Ingawa mko nchi ya mbali mkumbukeni Mwenyezi-Mungu, ukumbukeni pia mji wa Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wewe uliyepona upanga, ondoka wala usikawie! Mkumbuke Mwenyezi Mungu ukiwa katika nchi ya mbali, na utafakari juu ya Yerusalemu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ninyi mliojiepusha na upanga, Enendeni zenu, msisimame; Mkumbukeni Bwana tokea mbali, Na Yerusalemu ukatiwe mioyoni mwenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nyinyi mlinusurika kifo, ondokeni sasa, wala msisitesite! Ingawa mko nchi ya mbali mkumbukeni Mwenyezi-Mungu, ukumbukeni pia mji wa Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wewe uliyepona upanga, ondoka wala usikawie! Mkumbuke BWANA ukiwa katika nchi ya mbali, na utafakari juu ya Yerusalemu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wewe uliyepona upanga, ondoka wala usikawie! Mkumbuke bwana ukiwa katika nchi ya mbali, na utafakari juu ya Yerusalemu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ninyi mliojiepusha na upanga, Nendeni zenu, msisimame; Mkumbukeni BWANA tokea mbali, Na Yerusalemu ukatiwe mioyoni mwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nyinyi mlinusurika kifo, ondokeni sasa, wala msisitesite! Ingawa mko nchi ya mbali mkumbukeni Mwenyezi-Mungu, ukumbukeni pia mji wa Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninyi mliozikimbia panga, nendeni tu msisimame! Nako katika nchi za mbali mkumbukeni Bwana! Nao Yerusalemu na uingie mioyoni mwenu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ninyi mliojiepusha na upanga, Enendeni zenu, msisimame; Mkumbukeni BWANA tokea mbali, Na Yerusalemu ukatiwe mioyoni mwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi mulioponyoka kifo, muondoke sasa, wala musisitesite! Ingawa muko katika inchi ya mbali, mumukumbuke Yawe, muukumbuke vilevile Yerusalema.