Jeremiah 51:57 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitawalewesha wakuu na wenye hekima wake, watawala wake, madiwani na askari wake; watalala usingizi wa milele wasiinuke tena. Nasema mimi mfalme ambaye jina langu ni Mwenyezi-Mungu wa Majeshi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawafanya maafisa wake na wenye busara walewe, watawala wao, maafisa, pamoja na mashujaa wao; watalala milele na hawataamka,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, maliwali wake, na maakida wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, Bwana wa majeshi, ambaye jina lake ni Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitawalewesha wakuu na wenye hekima wake, watawala wake, madiwani na askari wake; watalala usingizi wa milele wasiinuke tena. Nasema mimi mfalme ambaye jina langu ni Mwenyezi-Mungu wa Majeshi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawafanya maafisa wake na wenye busara walewe, watawala wao, maafisa, pamoja na wapiganaji wao; watalala milele na hawataamka,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA Mwenye Nguvu Zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawafanya maafisa wake na wenye busara walewe, watawala wao, maafisa, pamoja na wapiganaji wao; watalala milele na hawataamka,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni bwana Mwenye Nguvu Zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, watawala wake, na makamanda wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitawalewesha wakuu na wenye hekima wake, watawala wake, madiwani na askari wake; watalala usingizi wa milele wasiinuke tena. Nasema mimi mfalme ambaye jina langu ni Mwenyezi-Mungu wa Majeshi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, nitakapowalevya wakuu wake na werevu wake wa kweli na watawala nchi wake na wajumbe wake na wapiga vita wake, walale usingizi wa kale na kale, wasiamke tena; ndivyo, asemavyo Mfalme, Bwana Mwenye vikosi ni Jina lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, maliwali wake, na maakida wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawalewesha wakubwa na wenye hekima wake, watawala wake, maliwali na waaskari wake; watalala usingizi wa milele wala hawataweza tena kuamuka. –Ni ujumbe wa mufalme, jina lake Yawe wa majeshi!