Jeremiah 51:58 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi Mwenyezi-Mungu wa Majeshi nasema: Ukuta mpana wa Babuloni utabomolewa mpaka chini, na malango yake marefu yatateketezwa kwa moto. Watu wanafanya juhudi za bure, mataifa yanajichosha maana mwisho wao ni motoni!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Ukuta mnene wa Babeli utasawazishwa, na malango yaliyoinuka yatateketezwa kwa moto; mataifa yanajichosha bure, taabu ya mataifa ni nishati tu ya miali ya moto.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana wa majeshi asema hivi, Kuta pana za Babeli zitabomolewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa; nao watu watajitaabisha kwa ubatili, na mataifa kwa moto; nao watachoka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi Mwenyezi-Mungu wa Majeshi nasema: Ukuta mpana wa Babuloni utabomolewa mpaka chini, na malango yake marefu yatateketezwa kwa moto. Watu wanafanya juhudi za bure, mataifa yanajichosha maana mwisho wao ni motoni!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Ukuta mnene wa Babeli utasawazishwa, na malango yaliyoinuka yatateketezwa kwa moto; mataifa yanajichosha bure, taabu ya mataifa ni nishati tu kwa ajili ya miali ya moto.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Ukuta mnene wa Babeli utasawazishwa, na malango yaliyoinuka yatateketezwa kwa moto; mataifa yanajichosha bure, taabu ya mataifa ni nishati tu ya miali ya moto.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA wa majeshi asema hivi, Kuta pana za Babeli zitabomolewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa; nao watu watajitaabisha kwa ubatili, na mataifa kwa moto; nao watachoka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi Mwenyezi-Mungu wa Majeshi nasema: Ukuta mpana wa Babuloni utabomolewa mpaka chini, na malango yake marefu yatateketezwa kwa moto. Watu wanafanya juhudi za bure, mataifa yanajichosha maana mwisho wao ni motoni!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Kuta za boma la Babeli, zingawa ni nene, zitabomolewa mpaka chini, nayo malango yake, yangawa ni marefu, yatateketezwa kwa moto. Koo za watu husumbukia mambo ya bure, nayo makabila hujichokesha kwa ajili ya moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA wa majeshi asema hivi, Kuta pana za Babeli zitabomolewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa; nao watu watajitaabisha kwa ubatili, na mataifa kwa moto; nao watachoka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe wa majeshi anasema hivi: Ukuta mukubwa wa Babeli utabomolewa mpaka chini, na milango yake mirefu itateketezwa kwa moto. Watu wanafanya juhudi za bure, mataifa yanajichokesha, maana mwisho wao ni katika moto!