Jeremiah 51:59 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo mwaka wa nne wa utawala wake, mfalme Sedekia alikwenda Babuloni pamoja na ofisa wa askari wake aitwaye Seraya mwana wa Neria na mjukuu wa Maseya. Kutokana na fursa hiyo mimi Yeremia nilimpa Seraya ujumbe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huu ndio ujumbe ambao nabii Yeremia alimpa msimamizi wa nyumba ya mfalme, Seraya mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, alipokwenda Babeli pamoja na Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa utawala wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Neno ambalo Yeremia, nabii, alimwamuru Seraya, mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, alipokwenda Babeli pamoja na Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa kumiliki kwake. Basi Seraya alikuwa msimamizi mkuu wa nyumba ya mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo mwaka wa nne wa utawala wake, mfalme Sedekia alikwenda Babuloni pamoja na ofisa wa askari wake aitwaye Seraya mwana wa Neria na mjukuu wa Maseya. Kutokana na fursa hiyo mimi Yeremia nilimpa Seraya ujumbe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huu ndio ujumbe Yeremia aliompa afisa Seraya mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, alipokwenda Babeli pamoja na Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa utawala wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huu ndio ujumbe Yeremia aliompa afisa Seraya mwana wa Neria mwana wa Maaseya, alipokwenda Babeli pamoja na Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa utawala wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Neno ambalo Yeremia, nabii, alimwamuru Seraya, mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, alipokwenda Babeli pamoja na Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa kumiliki kwake. Basi Seraya alikuwa msimamizi mkuu wa nyumba ya mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnamo mwaka wa nne wa utawala wake, mfalme Sedekia alikwenda Babuloni pamoja na ofisa wa askari wake aitwaye Seraya mwana wa Neria na mjukuu wa Maseya. Kutokana na fursa hiyo mimi Yeremia nilimpa Seraya ujumbe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hili ndilo neno, mfumbuaji Yeremia alilomwagizia Seraya, mwana wa Neria, mwana wa Masea, alipokwenda Babeli pamoja na mfalme Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa ufalme wake; naye Seraya alikuwa mkuu wa makambi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Neno ambalo Yeremia, nabii, alimwamuru Seraya, mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, alipokwenda Babeli pamoja na Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa kumiliki kwake. Basi Seraya alikuwa msimamizi mkuu wa nyumba ya mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa ine wa utawala wake, mufalme Zedekia alikwenda Babeli pamoja na mukubwa wa wasimamizi wa nyumba yake anayeitwa Seraya mwana wa Neria na mujukuu wa Maseya. Wakati huo mimi Yeremia nilimutolea Seraya ujumbe.