Jeremiah 51:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Babuloni ilikuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa Mwenyezi-Mungu, ambacho kiliilewesha dunia nzima. Mataifa yalikunywa divai yake, hata yakapatwa wazimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Babeli alikuwa kikombe cha dhahabu katika mkono wa Mwenyezi Mungu; aliufanya ulimwengu wote ulewe. Mataifa walikunywa mvinyo wake; kwa hiyo sasa wameingiwa na wazimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Babeli umekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa Bwana; kilicholevya dunia yote; mataifa wamekunywa mvinyo wake; kwa sababu hiyo mataifa wameingiwa na wazimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Babuloni ilikuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa Mwenyezi-Mungu, ambacho kiliilewesha dunia nzima. Mataifa yalikunywa divai yake, hata yakapatwa wazimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Babeli alikuwa kikombe cha dhahabu katika mkono wa BWANA; aliufanya ulimwengu wote ulewe. Mataifa walikunywa mvinyo wake; kwa hiyo sasa wameingiwa na wazimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Babeli alikuwa kikombe cha dhahabu katika mkono wa bwana; aliufanya ulimwengu wote ulewe. Mataifa walikunywa mvinyo wake; kwa hiyo sasa wameingiwa na wazimu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Babeli umekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa BWANA; kilicholevya dunia yote; mataifa wamekunywa mvinyo wake; kwa sababu hiyo mataifa wameingiwa na wazimu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Babuloni ilikuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa Mwenyezi-Mungu, ambacho kiliilewesha dunia nzima. Mataifa yalikunywa divai yake, hata yakapatwa wazimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Babeli ulikuwa kinyweo cha dhahabu mkononi mwa Bwana kilichozilevya nchi zote; mvinyo yake mataifa yaliinywa, kwa hiyo mataifa yakaingiwa na wazimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Babeli umekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa BWANA; kilicholevya dunia yote; mataifa wamekunywa mvinyo wake; kwa sababu hiyo mataifa wameingiwa na wazimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Babeli ilikuwa kikombe cha zahabu katika mukono wa Yawe, ambacho kiliilewesha dunia nzima. Mataifa yalikunywa divai yake; kwa hiyo, yakapata wazimu.