Jeremiah 51:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tulijaribu kuuponya Babuloni, lakini hauwezi kuponywa. Uacheni, twendeni zetu, kila mmoja katika nchi yake, maana hukumu yake ni kuu mno imeinuka mpaka mawinguni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Tungemponya Babeli, lakini hawezi kuponyeka; tumwacheni, na kila mmoja wetu aende nchi yake mwenyewe, kwa kuwa hukumu yake inafika angani, inapanda juu hadi mawinguni.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikilia mawinguni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tulijaribu kuuponya Babuloni, lakini hauwezi kuponywa. Uacheni, twendeni zetu, kila mmoja katika nchi yake, maana hukumu yake ni kuu mno imeinuka mpaka mawinguni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Tungemponya Babeli, lakini hawezi kuponyeka; tumwache na kila mmoja aende kwenye nchi yake mwenyewe, kwa kuwa hukumu yake inafika angani, inapanda juu mpaka mawinguni.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Tungemponya Babeli, lakini hawezi kuponyeka; tumwacheni, na kila mmoja wetu aende nchi yake mwenyewe, kwa kuwa hukumu yake inafika angani, inapanda juu hadi mawinguni.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikia mawinguni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tulijaribu kuuponya Babuloni, lakini hauwezi kuponywa. Uacheni, twendeni zetu, kila mmoja katika nchi yake, maana hukumu yake ni kuu mno imeinuka mpaka mawinguni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tulitaka kuuponya Babeli, lakini haukuponyeka; basi, uacheni, twende kila mtu katika nchi ya kwao! Kwani hukumu yake inafika hata mbinguni, inakwenda juu mpaka kwenye mawingu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikilia mawinguni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tulijaribu kuuponyesha Babeli, lakini hauwezi kupona. Muuache, tujiendee, kila mumoja katika inchi yake. Hukumu yake ni kubwa sana inafika mpaka katika mawingu.