Jeremiah 52:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha aliyangoa macho ya Sedekia na kumfunga pingu, akamchukua Sedekia Babuloni na kumtia kizuizini mpaka siku alipokufa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akayang’oa macho ya Sedekia, akamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli, alipomweka gerezani hadi siku ya kifo chake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akampofusha macho Sedekia; tena mfalme wa Babeli akamfunga kwa pingu, akamchukua mpaka Babeli, akamtia gerezani hata siku ya kufa kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha aliyang'oa macho ya Sedekia na kumfunga pingu, akamchukua Sedekia Babuloni na kumtia kizuizini mpaka siku alipokufa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akayang'oa macho ya Sedekia, akamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli alipomweka gerezani mpaka siku ya kifo chake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akayang’oa macho ya Sedekia, akamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli, alipomweka gerezani mpaka siku ya kifo chake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akampofusha macho Sedekia; tena mfalme wa Babeli akamfunga kwa pingu, akamchukua mpaka Babeli, akamtia gerezani hata siku ya kufa kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha aliyangoa macho ya Sedekia na kumfunga pingu, akamchukua Sedekia Babuloni na kumtia kizuizini mpaka siku alipokufa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akayapofua macho yake Sedekia, akamfunga kwa minyororo; kisha mfalme wa Babeli akampeleka Babeli, akamtia kifungoni mpaka siku ya kufa kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akampofusha macho Sedekia; tena mfalme wa Babeli akamfunga kwa pingu, akamchukua mpaka Babeli, akamtia gerezani hata siku ya kufa kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha aliyaongoa macho ya Zedekia na kumufunga minyororo, akamupeleka Zedekia Babeli na kumutia katika kifungo mpaka siku alipokufa.