Jeremiah 52:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakaldayo walivunja vipandevipande nguzo za shaba nyeusi ambazo zilikuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu pamoja na vikalio na birika kubwa la shaba nyeusi lililokuwamo katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakaichukua shaba nyeusi yote mpaka Babuloni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaldayo walivunja nguzo za shaba, vishikilio vya shaba, na Bahari ya shaba, ambavyo vyote vilikuwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Kisha wakaichukua shaba yote wakaipeleka Babeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na nguzo za shaba zilizokuwa katika nyumba ya Bwana, na matako ya bahari ya shaba iliyokuwa katika nyumba ya Bwana, Wakaldayo walivivunja vipande vipande, wakaichukua shaba yake yote mpaka Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakaldayo walivunja vipandevipande nguzo za shaba nyeusi ambazo zilikuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu pamoja na vikalio na birika kubwa la shaba nyeusi lililokuwamo katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakaichukua shaba nyeusi yote mpaka Babuloni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaldayo walivunja nguzo za shaba, vile vibanio vinavyohamishika na ile Bahari ya Shaba ambavyo vyote vilikuwa katika Hekalu la BWANA, wakachukua shaba yote na kuipeleka Babeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaldayo walivunja vipande zile nguzo za shaba, vile vishikilio vya shaba vilivyohamishika, na ile Bahari ya shaba, ambavyo vyote vilikuwa katika Hekalu la bwana. Hivyo wakaichukua hiyo shaba yote na kuipeleka Babeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na nguzo za shaba zilizokuwa katika nyumba ya BWANA, na vikalio vya mazulia ya shaba iliyokuwa katika nyumba ya BWANA, Wakaldayo walivivunja vipande vipande, wakaichukua shaba yake yote mpaka Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakaldayo walivunja vipandevipande nguzo za shaba nyeusi ambazo zilikuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu pamoja na vikalio na birika kubwa la shaba nyeusi lililokuwamo katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakaichukua shaba nyeusi yote mpaka Babuloni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini zile nguzo mbili za shaba zilizokuwa penye Nyumba ya Bwana na vile vilingo vya kuwekea mitungi ya maji na bahari ya shaba iliyokuwa penye Nyumba ya Bwana Wakasidi wakazivunja, nazo zile shaba zao zote wakazipeleka Babeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na nguzo za shaba zilizokuwa katika nyumba ya BWANA, na matako ya bahari ya shaba iliyokuwa katika nyumba ya BWANA, Wakaldayo walivivunja vipande vipande, wakaichukua shaba yake yote mpaka Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaldea walivunja vipandevipande nguzo za shaba nyeusi ambazo zilikuwa katika nyumba ya Yawe pamoja na misingi ya birika kubwa la shaba nyeusi lililokuwa katika nyumba ya Yawe, wakapeleka shaba nyeusi yote mpaka Babeli.