Jeremiah 52:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kadhalika, walichukua vyungu, sepetu, mikasi, makarai, vijiko vikubwa na vyombo vyote vya shaba nyeusi vilivyotumiwa katika huduma ya hekalu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakachukua pia vyungu, masepetu, mikasi ya kusawazishia tambi, mabakuli ya kunyunyizia, sahani na vyombo vyote vya shaba vilivyotumika Hekaluni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayo masufuria, na majembe, na makasi, na mabakuli, na miiko, na vyombo vyote vya shaba walivyokuwa wakivitumia, wakavichukua vyote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kadhalika, walichukua vyungu, sepetu, mikasi, makarai, vijiko vikubwa na vyombo vyote vya shaba nyeusi vilivyotumiwa katika huduma ya hekalu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walichukua pia zile sufuria, yale masepetu, ile mikasi ya kusawazishia tambi, yale mabakuli ya kunyunyizia, sahani pamoja na vyombo vyote vya shaba vilivyotumika ndani ya Hekalu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakachukua pia vyungu, masepetu, mikasi ya kusawazishia tambi, mabakuli ya kunyunyizia, sahani na vyombo vyote vya shaba vilivyotumika katika huduma ya Hekalu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nayo masufuria, na majembe, na makasi, na mabakuli, na miiko, na vyombo vyote vya shaba walivyokuwa wakivitumia, wakavichukua vyote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kadhalika, walichukua vyungu, sepetu, mikasi, makarai, vijiko vikubwa na vyombo vyote vya shaba nyeusi vilivyotumiwa katika huduma ya hekalu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata masufuria na majembe na makato ya kusafishia mishumaa na vyano na kata navyo vyombo vyote pia vya shaba vilivyotumiwa Nyumbani mwa Bwana wakavichukua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayo masufuria, na majembe, na makasi, na mabakuli, na miiko, na vyombo vyote vya shaba walivyokuwa wakivitumia, wakavichukua vyote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile, walipeleka vyungu, majembe, makasi, makarai, vijiko vikubwa na vyombo vyote vya shaba nyeusi vilivyotumiwa katika kazi ya hekalu.