Jeremiah 52:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhusu vitu Solomoni alivyotengeneza: Nguzo mbili, birika kubwa moja na sanamu za fahali kumi na mbili za shaba nyeusi ambazo zilikuwa chini ya hilo birika kubwa pamoja na vikalio, shaba nyeusi ya vitu hivi vyote ilikuwa na uzito mwingi sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Shaba iliyotokana na zile nguzo mbili, ile Bahari na wale mafahali kumi na wawili wa shaba waliokuwa chini yake, pamoja na vile vishikilio vilivyohamishika, ambavyo Mfalme Sulemani alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, ilikuwa na uzito mwingi usioweza kupimika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nguzo mbili, bahari moja, na ng'ombe kumi na mbili za shaba zilizokuwa chini ya matako yake, ambavyo mfalme Sulemani aliifanyia nyumba ya Bwana; shaba ya vitu hivyo vyote ilikuwa haiwezi kupimwa kwa kuwa nyingi sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhusu vitu Solomoni alivyotengeneza: nguzo mbili, birika kubwa moja na sanamu za fahali kumi na mbili za shaba nyeusi ambazo zilikuwa chini ya hilo birika kubwa pamoja na vikalio, shaba nyeusi ya vitu hivi vyote ilikuwa na uzito mwingi sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Shaba iliyotokana na zile nguzo mbili, ile Bahari na wale mafahali kumi na mawili wa shaba waliokuwa chini yake, pamoja na vile vibanio vinavyohamishika, ambavyo Mfalme Solomoni alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Hekalu la BWANA, vilikuwa na uzito usioweza kupimika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Shaba iliyotokana na zile nguzo mbili, ile Bahari na wale mafahali kumi na mawili wa shaba waliokuwa chini yake, pamoja na vile vishikilio vilivyohamishika, ambavyo Mfalme Sulemani alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Hekalu la bwana, ilikuwa na uzito usioweza kupimika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nguzo mbili, beseni, na ng'ombe kumi na mbili za shaba zilizokuwa chini ya vikalio vyake, ambavyo mfalme Sulemani aliifanyia nyumba ya BWANA; shaba ya vitu hivyo vyote ilikuwa haiwezi kupimwa kwa kuwa nyingi sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhusu vitu Solomoni alivyotengeneza: Nguzo mbili, birika kubwa moja na sanamu za fahali kumi na mbili za shaba nyeusi ambazo zilikuwa chini ya hilo birika kubwa pamoja na vikalio, shaba nyeusi ya vitu hivi vyote ilikuwa na uzito mwingi sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Zile nguzo mbili na ile bahari moja na zile ng'ombe kumi na mbili zilizokuwa chini yake na vile vilingo vya kuwekea mitungi ya maji, ambavyo mfalme Salomo alivitengenezea Nyumba ya Bwana, shaba zao hivyo vyombo vyote hazikuwezekana kupimwa kwa mizani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nguzo mbili, bahari moja, na ng’ombe kumi na mbili za shaba zilizokuwa chini ya matako yake, ambavyo mfalme Sulemani aliifanyia nyumba ya BWANA; shaba ya vitu hivyo vyote ilikuwa haiwezi kupimwa kwa kuwa nyingi sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Juu ya vitu Solomono alivyotengeneza: nguzo mbili, birika kubwa moja na sanamu za ngombe dume kumi na mbili za shaba nyeusi ambazo zilikuwa chini ya hilo birika kubwa pamoja na misingi, shaba nyeusi ya vitu hivi vyote ilikuwa na uzito mwingi sana.