Jeremiah 52:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na kutoka mjini alimchukua ofisa mmoja ambaye alikuwa akiongoza askari vitani, pamoja na watu saba washauri wa mfalme ambao aliwakuta mjini. Kadhalika alimchukua katibu wa kamanda mkuu wa jeshi ambaye alitunza kumbukumbu za jeshi pamoja na watu mashuhuri sitini ambao aliwakuta mjini Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Miongoni mwa wale watu waliokuwa wamesalia katika mji, alimchukua afisa kiongozi wa wapiganaji, na washauri saba wa mfalme. Akamchukua pia mwandishi aliyesimamia uandikishaji wa watu wa nchi, pamoja na watu wake sitini waliopatikana ndani ya mji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na katika mji akatwaa towashi mmoja aliyewasimamia watu wa vita; na watu saba katika wale waliouona uso wa mfalme, walioonekana katika mji; na karani wa jemadari wa jeshi, aliyewaandika watu wa nchi; na watu sitini katika watu wa nchi, walioonekana ndani ya mji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na kutoka mjini alimchukua ofisa mmoja ambaye alikuwa akiongoza askari vitani, pamoja na watu saba washauri wa mfalme ambao aliwakuta mjini. Kadhalika alimchukua katibu wa kamanda mkuu wa jeshi ambaye alitunza kumbukumbu za jeshi pamoja na watu mashuhuri sitini ambao aliwakuta mjini Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Miongoni mwa wale watu waliokuwa wamesalia katika mji, alimchukua afisa kiongozi wa wapiganaji na washauri saba wa kifalme. Akamchukua pia mwandishi aliyekuwa afisa mkuu wa kuandika watu wa nchi na watu wake sitini waliokutwa katika mji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Miongoni mwa wale watu waliokuwa wamesalia katika mji, alimchukua afisa kiongozi wa wapiganaji, na washauri saba wa mfalme. Akamchukua pia mwandishi aliyesimamia uandikishaji wa watu wa nchi, pamoja na watu wake sitini waliopatikana ndani ya mji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na katika mji akatwaa towashi mmoja aliyewasimamia watu wa vita; na watu saba katika wale waliouona uso wa mfalme, walioonekana katika mji; na karani wa jemadari wa jeshi, aliyewaandika watu wa nchi; na watu sitini katika watu wa nchi, walioonekana ndani ya mji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na kutoka mjini alimchukua ofisa mmoja ambaye alikuwa akiongoza askari vitani, pamoja na watu saba washauri wa mfalme ambao aliwakuta mjini. Kadhalika alimchukua katibu wa kamanda mkuu wa jeshi ambaye alitunza kumbukumbu za jeshi pamoja na watu mashuhuri sitini ambao aliwakuta mjini Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo mjini akachukua mtumishi mmoja wa nyumbani mwa mfalme aliyewekwa kuwa mkuu wa kuwasimamia wapiga vita na watu saba waliokuwa na kazi machoni pa mfalme waliopatikana mjini na mwandishi wa mkuu wa vikosi aliyewaandika watu wa nchi waliotakiwa uaskari na watu sitini wa shambani waliopatikana mle mjini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na katika mji akatwaa towashi mmoja aliyewasimamia watu wa vita; na watu saba katika wale waliouona uso wa mfalme, walioonekana katika mji; na karani wa jemadari wa jeshi, aliyewaandika watu wa nchi; na watu sitini katika watu wa nchi, walioonekana ndani ya mji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kutoka katika muji alimukamata mukubwa mumoja ambaye alikuwa akiongoza waaskari katika vita, pamoja na watu saba washauri wa mufalme ambao aliwakuta katika muji. Alimukamata vilevile katibu wa jemadari mukubwa wa waaskari ambaye alishugulika na kazi ya kuandika waaskari wapya, pamoja na watu wakubwa makumi sita ambao aliwakuta katika muji Yerusalema.