Jeremiah 52:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wake Nebukadneza, Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, alichukua mateka Wayahudi 745. Jumla ya mateka wote ilikuwa watu 4,600.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
katika mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wake, Wayahudi mia saba na arobaini na watano (745) walichukuliwa kwenda uhamishoni na Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi wa mfalme. Jumla ya watu wote walikuwa elfu nne mia sita.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
katika mwaka wa ishirini na tatu wa Nebukadreza, Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawachukua mateka katika Wayahudi watu mia saba na arobaini na watano; jumla ya watu hao wote ni watu elfu nne na mia sita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wake Nebukadneza, Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, alichukua mateka Wayahudi 745. Jumla ya mateka wote ilikuwa watu 4,600.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
katika mwaka wa ishirini na tatu wa kutawala kwake, Wayahudi 745 walichukuliwa kwenda uhamishoni na Nebuzaradani, jemadari wa askari walinzi wa mfalme. Jumla ya watu wote walikuwa 4,600.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
katika mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wake, Wayahudi 745 walichukuliwa kwenda uhamishoni na Nebuzaradani jemadari wa askari walinzi wa mfalme. Jumla ya watu wote walikuwa 4,600.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
katika mwaka wa ishirini na tatu wa Nebukadneza, Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, akawachukua mateka katika Wayahudi watu mia saba na arobaini na watano; jumla ya watu hao wote ni watu elfu nne na mia sita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wake Nebukadneza, Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, alichukua mateka Wayahudi 745. Jumla ya mateka wote ilikuwa watu 4,600.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwaka wa ishirini na tatu wa ufalme wa Nebukadinesari, Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, akahamisha Wayuda 745; wote pamoja walikuwa 4600.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
katika mwaka wa ishirini na tatu wa Nebukadreza, Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawachukua mateka katika Wayahudi watu mia saba na arobaini na watano; jumla ya watu hao wote ni watu elfu nne na mia sita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwaka wa makumi mbili na tatu wa utawala wa Nebukadneza, Nebuzaradani mukubwa wa waaskari walinzi wa mufalme, aliwapeleka Wayuda mia saba na makumi ine na watano. Jumla ya watu wote ilikuwa watu elfu ine mia sita.