Jeremiah 6:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, waliona aibu walipofanya machukizo hayo? La! Hawakuona aibu hata kidogo. Hawakujua hata namna ya kuona aibu. Kwa hiyo wataanguka pamoja na wale waangukao; wakati nitakapowaadhibu, wataangamizwa kabisa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao inayochukiza mno? Hapana, hawana haya hata kidogo; hawajui hata kuona aibu. Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka, watashushwa chini nitakapowaadhibu,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Walitahayarika, walipokuwa wameunda machukizo? La, hawakutahayarika hata kidogo, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi, wataanguka miongoni mwa hao waangukao; wakati nitakapowajilia wataangushwa chini, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, waliona aibu walipofanya machukizo hayo? La! Hawakuona aibu hata kidogo. Hawakujua hata namna ya kuona aibu. Kwa hiyo wataanguka pamoja na wale waangukao; wakati nitakapowaadhibu, wataangamizwa kabisa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao inayochukiza mno? Hapana, hawana aibu hata kidogo; hawajui hata kuona haya. Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka, watashushwa nitakapowaadhibu,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao inayochukiza mno? Hapana, hawana aibu hata kidogo; hawajui hata kuona haya. Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka, watashushwa chini nitakapowaadhibu,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Walitahayarika, walipokuwa wameunda machukizo? La, hawakutahayarika hata kidogo, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi, wataanguka miongoni mwa hao waangukao; wakati nitakapowajia wataangushwa chini, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, waliona aibu walipofanya machukizo hayo? La! Hawakuona aibu hata kidogo. Hawakujua hata namna ya kuona aibu. Kwa hiyo wataanguka pamoja na wale waangukao; wakati nitakapowaadhibu, wataangamizwa kabisa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watapatwa na soni, kwani hufanya yatapishayo; lakini hawaoni soni, wala hawajui kuiva nyuso. Kwa hiyo wataanguka pamoja na wenzao watakaoanguka siku hiyo, nitakapowapatiliza; ndipo, watakapojikwaa. Ndivyo, Bwana anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Walitahayarika, walipokuwa wameunda machukizo? La, hawakutahayarika hata kidogo, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi, wataanguka miongoni mwa hao waangukao; wakati nitakapowajilia wataangushwa chini, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wao walisikia haya walipofanya machukizo hayo? Hapana! Hawakusikia haya hata kidogo. Hata zamiri hazikuwagonga. Kwa hiyo wataanguka pamoja na wale wanaoanguka; wakati nitakapowaazibu, wataangamizwa kabisa. –Ni Yawe anayesema hivyo.