Jeremiah 6:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wamezishika pinde zao na mikuki, watu wakatili wasio na huruma. Vishindo vyao ni kama ngurumo ya bahari. Wamepanda farasi, wamejipanga tayari kwa vita, dhidi yako ewe Siyoni!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wamejifunga pinde na mkuki, ni wakatili na hawana huruma. Wanatoa sauti kama bahari inayounguruma wanapoendesha farasi wao. Wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita ili kukushambulia, ee Binti Sayuni.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Washika upinde na mkuki; ni wakatili, hawana huruma; sauti yao huvuma kama bahari, nao wamepanda farasi zao; kila mmoja kama mtu wa vita amejipanga juu yako, Ee binti Sayuni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wamezishika pinde zao na mikuki, watu wakatili wasio na huruma. Vishindo vyao ni kama ngurumo ya bahari. Wamepanda farasi, wamejipanga tayari kwa vita, dhidi yako ewe Siyoni!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wamejifunga pinde na mkuki, ni wakatili na hawana huruma. Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma wanapokuwa wamepanda farasi zao, wanakuja kama watu walioandaliwa tayari kwa vita kukushambulia wewe, Ee Binti Sayuni.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wamejifunga pinde na mkuki, ni wakatili na hawana huruma. Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma wanapoendesha farasi zao. Wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita ili kukushambulia, ee Binti Sayuni.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Washika upinde na mkuki; ni wakatili, hawana huruma; sauti yao huvuma kama bahari, nao wamepanda farasi wao; kila mmoja kama mtu wa vita amejipanga juu yako, Ee binti Sayuni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wamezishika pinde zao na mikuki, watu wakatili wasio na huruma. Vishindo vyao ni kama ngurumo ya bahari. Wamepanda farasi, wamejipanga tayari kwa vita, dhidi yako ewe Siyoni!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hushika pindi na mikuki, ni wakorofi pasipo huruma, makelele yao ni kama kuvuma kwa bahari, nao hupanda farasi; wamejivika kama watu waendao vitani, wapigane na wewe, binti Sioni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Washika upinde na mkuki; ni wakatili, hawana huruma; sauti yao huvuma kama bahari, nao wamepanda farasi zao; kila mmoja kama mtu wa vita amejipanga juu yako, Ee binti Sayuni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wameshika pinde zao na mikuki; ni watu wakali wasiokuwa na huruma. Vishindo vyao ni kama uvumi wa bahari. Wamepanda juu ya farasi, wamejipanga tayari kwa vita na wewe Sayuni!