Jeremiah 6:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama kisima kinavyohifadhi maji yake yakabaki safi, ndivyo Yerusalemu unavyohifadhi uovu wako. Ukatili na uharibifu vyasikika ndani yake, magonjwa na majeraha yake nayaona daima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake, ndivyo anavyomwaga uovu wake. Ukatili na maangamizi vyasikika ndani yake, ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama vile kisima kitoavyo maji yake, ndivyo utoavyo uovu wake; jeuri na kuharibu kwasikiwa ndani yake; ugonjwa na jeraha zi mbele zangu daima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama kisima kinavyohifadhi maji yake yakabaki safi, ndivyo Yerusalemu unavyohifadhi uovu wako. Ukatili na uharibifu vyasikika ndani yake, magonjwa na majeraha yake nayaona daima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake, ndivyo anavyomwaga uovu wake. Ukatili na maangamizi yasikika ndani yake, ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake, ndivyo anavyomwaga uovu wake. Ukatili na maangamizi yasikika ndani yake, ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama vile kisima kitoavyo maji yake, ndivyo utoavyo uovu wake; jeuri na kuharibu kwasikiwa ndani yake; ugonjwa na jeraha zi mbele zangu daima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama kisima kinavyohifadhi maji yake yakabaki safi, ndivyo Yerusalemu unavyohifadhi uovu wako. Ukatili na uharibifu vyasikika ndani yake, magonjwa na majeraha yake nayaona daima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama kisima kinavyoyatoa maji yake, ndivyo, unavyoyatoa mabaya yake. Makorofi na mapotovu husikilika mwake, macho yangu huona siku zote maumivu na mapigo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama vile kisima kitoavyo maji yake, ndivyo utoavyo uovu wake; jeuri na kuharibu kwasikiwa ndani yake; ugonjwa na jeraha zi mbele zangu daima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama vile maji yanavyotiririka toka ndani ya kisima, ndivyo maovu yanavyotiririka katika Yerusalema. Mateso makali na maangamizi yanasikilika ndani yake. Ninaona magonjwa na vidonda mbele yangu kila siku.