Jeremiah 6:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Kusanyeni watu wote wa Israeli waliobaki kama watu wakusanyavyo zabibu zote; kama afanyavyo mchumazabibu, pitisheni tena mikono yenu katika matawi yake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Wao na wayakusanye mabaki ya Israeli kwa uangalifu kama kwenye mzabibu; pitisha mkono wako kwenye matawi tena, kama yeye avunaye zabibu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana wa majeshi asema hivi, Wataokota mabaki ya Israeli kama mzabibu; rudisha mkono wako ndani ya vikapu, kama mchuma zabibu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Kusanyeni watu wote wa Israeli waliobaki kama watu wakusanyavyo zabibu zote; kama afanyavyo mchumazabibu, pitisheni tena mikono yenu katika matawi yake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Wao na wayakusanye mabaki ya Israeli kwa uangalifu kama kwenye mzabibu; pitisha mkono wako kwenye matawi tena, kama yeye avunaye zabibu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivi ndivyo asemavyo bwana Mwenye Nguvu Zote: “Wao na wayakusanye mabaki ya Israeli kwa uangalifu kama kwenye mzabibu; pitisha mkono wako kwenye matawi tena, kama yeye avunaye zabibu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA wa majeshi asema hivi, Wataokota mabaki ya Israeli kama mzabibu; rudisha mkono wako ndani ya vikapu, kama mchuma zabibu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Kusanyeni watu wote wa Israeli waliobaki kama watu wakusanyavyo zabibu zote; kama afanyavyo mchumazabibu, pitisheni tena mikono yenu katika matawi yake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Masao yako, Isiraeli, yataokotezwa kama yake mzabibu; ukunjue tena mkono wako kama mchuma zabibu, akiyatazama matawi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA wa majeshi asema hivi, Wataokota mabaki ya Israeli kama mzabibu; rudisha mkono wako ndani ya vikapu, kama mchuma zabibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe wa majeshi anasema hivi: Muwakusanye watu wote wa Israeli waliobaki kama vile watu wanavyookotesha zabibu katika shamba; kama vile muchumaji wa zabibu, mupitishe mikono katikati ya matawi yote.