Jeremiah 7:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nendeni mahali pangu kule Shilo, mahali nilipopachagua niabudiwe hapo awali, mkaone maangamizi niliyoyafanya huko kwa sababu ya uovu wa watu wangu, Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Nendeni sasa mahali pangu palipokuwa huko Shilo, ambapo nilipafanya pa kwanza kuwa makao ya Jina langu, nanyi mwone lile nililopafanyia kwa ajili ya uovu wa watu wangu Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini enendeni sasa hata mahali pangu palipokuwapo katika Shilo, nilipolikalisha jina langu hapo kwanza, mkaone nilivyopatenda kwa sababu ya uovu wa watu wangu Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nendeni mahali pangu kule Shilo, mahali nilipopachagua niabudiwe hapo awali, mkaone maangamizi niliyoyafanya huko kwa sababu ya uovu wa watu wangu, Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Nendeni sasa mahali pangu palipokuwa huko Shilo, mahali ambapo nilipafanya pa kwanza kuwa makao ya Jina langu, nanyi mwone lile nililopafanyia kwa ajili ya uovu wa watu wangu Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Nendeni sasa mahali pangu palipokuwa huko Shilo, mahali ambapo nilipafanya pa kwanza kuwa makao ya Jina langu, nanyi mwone lile nililopafanyia kwa ajili ya uovu wa watu wangu Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini nendeni sasa hadi mahali pangu palipokuwapo katika Shilo, nilipolikalisha jina langu hapo kwanza, mkaone nilivyopatenda kwa sababu ya uovu wa watu wangu Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nendeni mahali pangu kule Shilo, mahali nilipopachagua niabudiwe hapo awali, mkaone maangamizi niliyoyafanya huko kwa sababu ya uovu wa watu wangu, Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya! Nendeni mahali pangu kule Silo, nilipolikalisha Jina langu kwanza, myaone yote, niliyopafanyizia kwa ajili ya ubaya wao Waisiraeli walio ukoo wangu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini enendeni sasa hata mahali pangu palipokuwapo katika Shilo, nilipolikalisha jina langu hapo kwanza, mkaone nilivyopatenda kwa sababu ya uovu wa watu wangu Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muende kwenye pahali pangu kule Shilo, nafasi nilipochagua kwa kuabudiwa mara ya kwanza, muone maangamizi niliyofanya kule kwa sababu ya uovu wa watu wangu, Israeli.