Jeremiah 7:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watoto huokota kuni, akina baba huwasha moto na akina mama hukanda unga ili waoke mikate kwa ajili ya mungu wa kike wanayemwita malkia wa mbinguni. Tena wanaimiminia miungu mingine tambiko ya divai ili kuniudhi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watoto wanakusanya kuni, baba zao wanawasha moto, na wanawake wanakanda unga na kuoka mikate kwa ajili ya Malkia wa Mbinguni. Wanamimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine ili kunikasirisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watoto huokota kuni, akina baba huwasha moto na akina mama hukanda unga ili waoke mikate kwa ajili ya mungu wa kike wanayemwita malkia wa mbinguni. Tena wanaimiminia miungu mingine tambiko ya divai ili kuniudhi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watoto wanakusanya kuni, baba zao wanawasha moto na wanawake wanakanda unga na kuoka mikate kwa ajili ya Malkia wa Mbinguni. Wanamimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine ili kunikasirisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watoto wanakusanya kuni, baba zao wanawasha moto, na wanawake wanakanda unga na kuoka mikate kwa ajili ya Malkia wa Mbinguni. Wanamimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine ili kunikasirisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watoto huokota kuni, akina baba huwasha moto na akina mama hukanda unga ili waoke mikate kwa ajili ya mungu wa kike wanayemwita malkia wa mbinguni. Tena wanaimiminia miungu mingine tambiko ya divai ili kuniudhi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watoto huokota kuni, nao baba huziwasha moto, wanawake wakikanda unga wa kufanya vikate vya mfalme wa kike wa mbinguni, tena humwaga vinywaji vya kutambikia miungu mingine, kusudi waniumize moyoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watoto wanaokota kuni, wababa wanawakisha moto na wamama wanaponda unga kwa ajili ya kutengeneza mikate ya kumutambikia mungu wa kike, wanayemwita malkia wa mbinguni. Tena wananikasirikisha kwa kuitolea miungu mingine sadaka ya divai.