Jeremiah 7:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini niliwapa amri hii: Waitii sauti yangu ili niwe Mungu wao, nao wawe watu wangu. Niliwaamuru pia waishi kama nilivyowaagiza, ili mambo yao yawaendee vema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
lakini niliwapa amri hii nikisema: Nitiini mimi, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Nendeni katika njia zote ninazowaamuru ili mpate kufanikiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini naliwaamuru neno hili, nikisema, Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu; mkaende katika njia ile yote nitakayowaamuru mpate kufanikiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini niliwapa amri hii: waitii sauti yangu ili niwe Mungu wao, nao wawe watu wangu. Niliwaamuru pia waishi kama nilivyowaagiza, ili mambo yao yawaendee vema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
lakini niliwapa amri hii nikisema: Mtanitii mimi, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Enendeni katika njia zote ninazowaamuru ili mpate kufanikiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
lakini niliwapa amri hii nikisema: Nitiini mimi, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Enendeni katika njia zote ninazowaamuru ili mpate kufanikiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini niliwaamuru neno hili, nikisema, Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu; mkaende katika njia ile yote nitakayowaamuru mpate kufanikiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini niliwapa amri hii: Waitii sauti yangu ili niwe Mungu wao, nao wawe watu wangu. Niliwaamuru pia waishi kama nilivyowaagiza, ili mambo yao yawaendee vema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli niliwaagiza neno hili tu kwamba: Isikieni sauti yangu! Ndivyo, nitakavyokuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa ukoo wangu. Kisha zishikeni njia zote, nitakazowaagiza, mpate kuona mema!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini naliwaamuru neno hili, nikisema, Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu; mkaende katika njia ile yote nitakayowaamuru mpate kufanikiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini niliwapa amri kwamba waitii sauti yangu kusudi nikuwe Mungu wao, nao wakuwe watu wangu. Niliwaamuru vilevile waishi kama nilivyowaagiza, kusudi wapate uheri.