Jeremiah 7:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Watu wa Yuda wametenda uovu mbele yangu. Wameweka vinyago vyao vya kuchukiza ndani ya nyumba hii ijulikanayo kwa jina langu, wakaitia unajisi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Watu wa Yuda wamefanya maovu machoni pangu, asema Mwenyezi Mungu. Wameziweka sanamu zao za machukizo ndani ya nyumba iitwayo kwa Jina langu, na wameitia unajisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana wana wa Yuda wametenda yaliyo maovu machoni pangu, asema Bwana; wameweka machukizo yao ndani ya nyumba hiyo, iitwayo kwa jina langu, hata kuitia unajisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Watu wa Yuda wametenda uovu mbele yangu. Wameweka vinyago vyao vya kuchukiza ndani ya nyumba hii ijulikanayo kwa jina langu, wakaitia unajisi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Watu wa Yuda wamefanya maovu machoni pangu, asema BWANA. Wameziweka sanamu zao za machukizo ndani ya nyumba iitwayo kwa Jina langu na wameitia unajisi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Watu wa Yuda wamefanya maovu machoni pangu, asema bwana. Wameziweka sanamu zao za machukizo ndani ya nyumba iitwayo kwa Jina langu, na wameitia unajisi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana wana wa Yuda wametenda yaliyo maovu machoni pangu, asema BWANA; wameweka machukizo yao ndani ya nyumba hiyo, iitwayo kwa jina langu, hata kuitia unajisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Watu wa Yuda wametenda uovu mbele yangu. Wameweka vinyago vyao vya kuchukiza ndani ya nyumba hii ijulikanayo kwa jina langu, wakaitia unajisi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ndivyo, asemavyo Bwana: Wana wa Yuda wamefanya yaliyo mabaya machoni pangu, wakaweka matapisho yao katika Nyumba hii inayoitwa kwa Jina langu, waichafue.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana wana wa Yuda wametenda yaliyo maovu machoni pangu, asema BWANA; wameweka machukizo yao ndani ya nyumba hiyo, iitwayo kwa jina langu, hata kuitia unajisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Yuda wametenda maovu mbele yangu. Wameweka sanamu zenye kuchukiza ndani ya nyumba hii inayojulikana kwa jina langu na kuichafua.