Jeremiah 8:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, waliona aibu walipotenda machukizo hayo? La hasha! Hawakuona aibu hata kidogo. Hata hawajui kuona haya. Kwa hiyo, wataanguka pamoja na wale walioanguka; nitakapowaadhibu, wataangamia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao inayochukiza mno? Hapana, hawana haya hata kidogo, hawajui hata kuona aibu. Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka, watashushwa chini watakapoadhibiwa, asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Walitahayarika, walipokuwa wametenda machukizo? La! Hawakutahayarika, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi wataanguka miongoni mwao waangukao; wakati wa kujiliwa kwao wataangushwa chini, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, waliona aibu walipotenda machukizo hayo? La hasha! Hawakuona aibu hata kidogo. Hata hawajui kuona haya. Kwa hiyo, wataanguka pamoja na wale walioanguka; nitakapowaadhibu, wataangamia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao inayochukiza mno? Hapana, hawana aibu hata kidogo, hawajui hata kuona haya. Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka, watashushwa chini watakapoadhibiwa, asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao inayochukiza mno? Hapana, hawana aibu hata kidogo, hawajui hata kuona haya. Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka, watashushwa chini watakapoadhibiwa, asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Waliona aibu, walipokuwa wametenda machukizo? La! Hawakuona aibu kabisa, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi wataanguka miongoni mwao waangukao; wakati wa kujiliwa kwao wataangushwa chini, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, waliona aibu walipotenda machukizo hayo? La hasha! Hawakuona aibu hata kidogo. Hata hawajui kuona haya. Kwa hiyo, wataanguka pamoja na wale walioanguka; nitakapowaadhibu, wataangamia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watapatwa na soni, kwani hufanya yatapishayo; lakini hawaoni soni, wala hawajui kuiva nyuso. Kwa hiyo wataanguka pamoja na wenzao watakaoanguka siku hiyo, nitakapowapatiliza; ndipo, watakapojikwaa; ndivyo, Bwana anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Walitahayarika, walipokuwa wametenda machukizo? La! Hawakutahayarika, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi wataanguka miongoni mwao waangukao; wakati wa kujiliwa kwao wataangushwa chini, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walisikia haya walipotenda machukizo hayo? Hapana, hawakusikia haya hata kidogo. Hata zamiri hazikuwagonga. Kwa hiyo, wataanguka pamoja na wale walioanguka; nitakapowaazibu, wataangamia. –Ni Yawe anayesema hivyo.