Jeremiah 8:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Nilipotaka kukusanya chochote kutoka kwao, sikupata zabibu hata moja juu ya mzabibu, sikupata tini zozote juu ya mtini; hata majani yao yamekauka. Hata nilichokuwa nimewapa kimetoweka.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Nitayaondoa mavuno yao, asema Mwenyezi Mungu. Hapatakuwa zabibu kwenye mzabibu. Hapatakuwa na tini kwenye mtini, na majani yake yatanyauka. Kile nilichowapa watanyang’anywa.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nitawaangamiza kabisa, asema Bwana; hapana zabibu katika mizabibu, wala tini katika mitini, hata jani lake litanyauka; na vitu vile nilivyowapa vitawapotea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Nilipotaka kukusanya chochote kutoka kwao, sikupata zabibu hata moja juu ya mzabibu, sikupata tini zozote juu ya mtini; hata majani yao yamekauka. Hata nilichokuwa nimewapa kimetoweka.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Nitayaondoa mavuno yao, asema BWANA. Hapatakuwepo zabibu kwenye mzabibu. Hapatakuwepo na tini kwenye mtini, majani yake yatanyauka. Kile nilichowapa watanyang'anywa.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Nitayaondoa mavuno yao, asema bwana. Hapatakuwepo zabibu kwenye mzabibu. Hapatakuwepo na tini kwenye mtini, majani yake yatanyauka. Kile nilichowapa watanyang’anywa.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nitawaangamiza kabisa, asema BWANA; hapana zabibu katika mizabibu, wala tini katika mitini, hata jani lake litanyauka; na vitu vile nilivyowapa vitawapotea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Nilipotaka kukusanya chochote kutoka kwao, sikupata zabibu hata moja juu ya mzabibu, sikupata tini zozote juu ya mtini; hata majani yao yamekauka. Hata nilichokuwa nimewapa kimetoweka.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Ninapotaka kuchuma kwao, mizabibu, haina zabibu, wala mikuyu haina kuyu, nayo majani yao inakuwa inanyauka; kwa hiyo nitatoa watu, wawaondoe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nitawaangamiza kabisa, asema BWANA; hapana zabibu katika mizabibu, wala tini katika mitini, hata jani lake litanyauka; na vitu vile nilivyowapa vitawapotea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilitaka kuchuma matunda kutoka kwao. –Ni ujumbe wa Yawe.– Lakini sikupata zabibu hata moja juu ya muzabibu, sikupata tini zozote juu ya muti wa tini; hata majani yao yamekauka. Hata nilichokuwa nimewapa kimetoweka.