Jeremiah 8:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sauti za farasi wao zinasikika, kwa mlio wa farasi wao wa vita, nchi nzima inatetemeka. Wanafika na kuiharibu nchi na vyote vilivyomo, kuangamiza mji pamoja na wote waishio humo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkoromo wa farasi wa adui umesikika kuanzia Dani, kwa mlio wa madume yao ya farasi, nchi yote inatetemeka. Wamekuja kuangamiza nchi na vyote vilivyomo, mji na wote wanaoishi ndani yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kutoka Dani kumesikiwa mkoromo wa farasi zake; nchi yote pia inatetemeka kwa sauti ya mlio wa farasi zake za vita; maana wamekuja, wamekula nchi na vyote vilivyomo; huo mji na wote wakaao ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sauti za farasi wao zinasikika, kwa mlio wa farasi wao wa vita, nchi nzima inatetemeka. Wanafika na kuiharibu nchi na vyote vilivyomo, kuangamiza mji pamoja na wote waishio humo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkoromo wa farasi za adui umesikika kuanzia Dani, kwa mlio wa madume yao ya farasi, nchi yote inatetemeka. Wamekuja kuangamiza nchi na vyote vilivyomo, mji na wote waishio ndani yake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkoromo wa farasi za adui umesikika kuanzia Dani, kwa mlio wa madume yao ya farasi, nchi yote inatetemeka. Wamekuja kuangamiza nchi na vyote vilivyomo, mji na wote waishio ndani yake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kutoka Dani kumesikiwa mkoromo wa farasi wake; nchi yote pia inatetemeka kwa sauti ya mlio wa farasi wake wa vita; maana wamekuja, wamekula nchi na vyote vilivyomo; huo mji na wote wakaao ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sauti za farasi wao zinasikika, kwa mlio wa farasi wao wa vita, nchi nzima inatetemeka. Wanafika na kuiharibu nchi na vyote vilivyomo, kuangamiza mji pamoja na wote waishio humo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Upande wa Dani kunasikilika, farasi wao wanavyofoka, kwa uvumi wa makelele yao walio wenye nguvu nchi hii yote inatetemeka; watakuja, wataila nchi nayo yote yaliyomo, miji pamoja nao wakaaamo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kutoka Dani kumesikiwa mkoromo wa farasi zake; nchi yote pia inatetemeka kwa sauti ya mlio wa farasi zake za vita; maana wamekuja, wamekula nchi na vyote vilivyomo; huo mji na wote wakaao ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kelele za farasi wa waadui zinasikilika tokea Dani, kwa mulio wa farasi wao wa vita, inchi nzima inatetemeka. Wanafika na kuharibu inchi na vyote vinavyokuwa ndani yake, kuangamiza muji pamoja na wote wanaokaa humo.