Jeremiah 8:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, hakuna dawa ya kupaka huko Gileadi? Je, hakuna mganga huko? Mbona basi watu wangu hawajaponywa?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, hakuna zeri ya kuponya katika Gileadi? Je, hakuna tabibu huko? Kwa nini basi hakuna uponyaji wa majeraha ya watu wangu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Hapana zeri katika Gileadi? Huko hakuna tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya ya binti ya watu wangu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, hakuna dawa ya kupaka huko Gileadi? Je, hakuna mganga huko? Mbona basi watu wangu hawajaponywa?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, hakuna zeri ya kuponya katika Gileadi? Je, hakuna tabibu huko? Kwa nini basi hakuna uponyaji wa majeraha ya watu wangu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, hakuna zeri ya kuponya katika Gileadi? Je, hakuna tabibu huko? Kwa nini basi hakuna uponyaji wa majeraha ya watu wangu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Hakuna marhamu katika Gileadi? Huko hakuna tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya ya binti ya watu wangu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, hakuna dawa ya kupaka huko Gileadi? Je, hakuna mganga huko? Mbona basi watu wangu hawajaponywa?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Haiko miti yenye dawa huko Gileadi? Wala hakuna mponya huko? Mbona wazaliwa wa ukoo wangu hawakupata kuponywa?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Hapana zeri katika Gileadi? Huko hakuna tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya ya binti ya watu wangu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakuna dawa ya kupakaa kule Gileadi? Hakuna muganga kule? Mbona basi watu wangu hawajaponyeshwa?