Jeremiah 8:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote waliobaki wa jamaa hii mbovu, mahali popote pale nilipowatawanya, wataona heri kufa kuliko kuishi. Ndivyo nisemavyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Popote nitakapowafukuzia, mabaki wote wa kizazi hiki kiovu watatamani kufa kuliko kuishi, asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kufa kutachaguliwa kuliko kuishi na mabaki yote waliosalia katika jamaa hii mbovu, waliosalia kila mahali nilikowafukuza, asema Bwana wa majeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote waliobaki wa jamaa hii mbovu, mahali popote pale nilipowatawanya, wataona heri kufa kuliko kuishi. Ndivyo nisemavyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Po pote nitakapowafukuzia, mabaki wote wa kizazi hiki kiovu watatamani kufa kuliko kuishi, asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Popote nitakapowafukuzia, mabaki wote wa kizazi hiki kiovu watatamani kufa kuliko kuishi, asema bwana Mwenye Nguvu Zote.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kufa kutachaguliwa kuliko kuishi na mabaki wote waliosalia katika jamaa hii mbovu, waliosalia kila mahali nilikowafukuza, asema BWANA wa majeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote waliobaki wa jamaa hii mbovu, mahali popote pale nilipowatawanya, wataona heri kufa kuliko kuishi. Ndivyo nisemavyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo masazo yote yatakayosazwa ya mlango huu mbaya yatapendezwa zaidi na kufa kuliko kuwapo mahali po pote, nilipowatupia hayo masazo; ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kufa kutachaguliwa kuliko kuishi na mabaki yote waliosalia katika jamaa hii mbovu, waliosalia kila mahali nilikowafukuza, asema BWANA wa majeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wote watakaobaki wa jamaa hii mbaya, pahali popote pale nilipowasambaza, wataona heri kufa kuliko kuishi. –Ni ujumbe wa Yawe wa majeshi.