Jeremiah 8:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata korongo anajua wakati wa kuhama; njiwa, mbayuwayu na koikoi, hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawa hawajui kitu juu ya amri zangu mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata korongo aliye angani anayajua majira yake yaliyoamriwa, nao njiwa, mbayuwayu na koikoi hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawajui Mwenyezi Mungu anachotaka kwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata korongo anajua wakati wa kuhama; njiwa, mbayuwayu na koikoi, hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawa hawajui kitu juu ya amri zangu mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata korongo aliyeko angani anayajua majira yake yaliyoamriwa, nao njiwa, mbayuwayu na koikoi hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawajui BWANA anachotaka kwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata korongo aliyeko angani anayajua majira yake yaliyoamriwa, nao njiwa, mbayuwayu na koikoi hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawajui bwana anachotaka kwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata korongo anajua wakati wa kuhama; njiwa, mbayuwayu na koikoi, hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawa hawajui kitu juu ya amri zangu mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye korongo wa angani huzijua siku zake, hata hua na kinega na mbayuwayu huzishika siku zao za kuja, lakini walio ukoo wangu hawayajui yampasayo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata korongo anajua wakati wa kuhama; njiwa, mbaruwayi na koikoi, wanajua nyakati zao za kurudi. Lakini hawa watu wangu hawajui maagizo ya Yawe.