Jeremiah 9:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitaililia na kuiomboleza milima; nitayaombolezea malisho nyikani, kwa sababu yamekauka kabisa, hakuna mtu apitaye mahali hapo. Hakusikiki tena sauti za ng'ombe; ndege na wanyama wamekimbia na kutoweka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitalia na kuomboleza kwa ajili ya milima na kuomboleza kuhusu malisho ya jangwani. Yamekuwa ukiwa, wala hakuna apitaye humo, milio ya ng’ombe haisikiki. Ndege wa angani wametoroka na wanyama wamekimbia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa milima nitalia na kulalama, Na kwa malisho ya nyikani nitafanya maombolezo; Kwa sababu yameteketea, hata hapana apitaye, Wala hapana awezaye kusikia sauti ya ng'ombe; Ndege wa angani, na wanyama wa mwituni, Wamekimbia, wamekwenda zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitaililia na kuiomboleza milima; nitayaombolezea malisho nyikani, kwa sababu yamekauka kabisa, hakuna mtu apitaye mahali hapo. Hakusikiki tena sauti za ng'ombe; ndege na wanyama wamekimbia na kutoweka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitalia na kuomboleza kwa ajili ya milima na kuomboleza kuhusu malisho ya jangwani. Yamekuwa ukiwa na wala hakuna apitaye humo, milio ya ng'ombe haisikiki. Ndege wa angani wameruka na wanyama wameondoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitalia na kuomboleza kwa ajili ya milima na kuomboleza kuhusu malisho ya jangwani. Yamekuwa ukiwa, wala hakuna apitaye humo, milio ya ng’ombe haisikiki. Ndege wa angani wametoroka na wanyama wamekimbia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa milima nitalia na kulalama, Na kwa malisho ya nyikani nitafanya maombolezo; Kwa sababu yameteketea, hata hakuna apitaye, Wala hapana awezaye kusikia sauti ya ng'ombe; Ndege wa angani, na wanyama wa mwituni, Wamekimbia, wamekwenda zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitaililia na kuiomboleza milima; nitayaombolezea malisho nyikani, kwa sababu yamekauka kabisa, hakuna mtu apitaye mahali hapo. Hakusikiki tena sauti za ng'ombe; ndege na wanyama wamekimbia na kutoweka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Milima nitaililia na kuiombolezea, nazo mbuga za nyikani nitazitungia wimbo wa kilio, kwani ziko peke yao, hakuna mtu apitaye hapo, hapasikiliki tena sauti za ng'ombe, hata ndege wa angani pamoja na nyama wa porini wamekimbia kwenda zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa milima nitalia na kulalama, Na kwa malisho ya nyikani nitafanya maombolezo; Kwa sababu yameteketea, hata hapana apitaye, Wala hapana awezaye kusikia sauti ya ng’ombe; Ndege wa angani, na wanyama wa mwituni, Wamekimbia, wamekwenda zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema: Nitaifanya Yerusalema kuwa mabomoko matupu, nitaifanya kuwa pango la mbweha; na miji ya Yuda nitaifanya kuwa jangwa, pahali pasipokaliwa na mutu yeyote.