Jeremiah 9:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nami nikauliza, “Je kuna mtu mwenye hekima kiasi cha kuweza kueleza mambo haya? Mwenyezi-Mungu aliongea na nani hata huyo aweze kutangaza kitu hicho? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa tupu kama jangwa hata hakuna mtu apitaye humo?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni mtu yupi aliye na hekima ya kutosha ayaelewe haya? Ni nani aliyefundishwa na Mwenyezi Mungu awezaye kuyaeleza haya? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa ukiwa kama jangwa ambapo hakuna awezaye kupita?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni nani aliye na hekima, apate kuelewa na haya? Tena ni nani ambaye kinywa cha Bwana kimesema naye, apate kuyatangaza? Nayo ni nini maana yake nchi hii kuharibika, na kuteketea kama nyika, asipite mtu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nami nikauliza, “Je kuna mtu mwenye hekima kiasi cha kuweza kueleza mambo haya? Mwenyezi-Mungu aliongea na nani hata huyo aweze kutangaza kitu hicho? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa tupu kama jangwa hata hakuna mtu apitaye humo?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni mtu yupi aliye na hekima ya kutosha ayaelewe haya? Ni nani aliyefundishwa na BWANA awezaye kuyaeleza haya? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa ukiwa kama jangwa ambapo hakuna awezaye kupita?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni mtu yupi aliye na hekima ya kutosha ayaelewe haya? Ni nani aliyefundishwa na bwana awezaye kuyaeleza haya? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa ukiwa kama jangwa ambapo hakuna awezaye kupita?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni nani aliye na hekima, apate kuelewa haya? Tena ni nani ambaye kinywa cha BWANA kimesema naye, apate kuyatangaza? Nayo ni nini maana yake nchi hii kuharibika, na kuteketea kama nyika, asipite mtu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nami nikauliza, “Je kuna mtu mwenye hekima kiasi cha kuweza kueleza mambo haya? Mwenyezi-Mungu aliongea na nani hata huyo aweze kutangaza kitu hicho? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa tupu kama jangwa hata hakuna mtu apitaye humo?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yuko nani aliye mwerevu wa kweli, ayatambue haya? Yuko nani, ambaye kinywa cha Bwana kilisema naye, ayatangaze, kama ni kwa sababu gani, nchi hii ikiangamia, iwe peke yake, pasipite mtu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni nani aliye na hekima, apate kuelewa na haya? Tena ni nani ambaye kinywa cha BWANA kimesema naye, apate kuyatangaza? Nayo ni nini maana yake nchi hii kuharibika, na kuteketea kama nyika, asipite mtu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akajibu na kusema hivi: Ni kwa sababu wamekataa kushika sheria yangu niliyowapa, wamekataa kutii sauti yangu na kufuata mapenzi yangu.