Jeremiah 9:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani, ambamo ningewaacha watu wangu na kwenda zangu.” Mwenyezi-Mungu asema: “Wote ni watu wazinzi, ni genge la watu wahaini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Laiti ningekuwa na nyumba ya kukaa wasafiri jangwani, ningewaacha watu wangu na kwenda mbali nao, kwa kuwa wote ni wazinzi, kundi la watu wadanganyifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani, kibanda cha wasafiri; nipate kuwaacha watu wangu, na kuondoka kwao! Maana wao ni wazinzi, wote pia, mkutano wa watu wenye hiana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani, ambamo ningewaacha watu wangu na kwenda zangu.” Mwenyezi-Mungu asema: “Wote ni watu wazinzi, ni genge la watu wahaini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Laiti ningekuwa na nyumba ya kukaa wasafiri katika jangwa, ningewaacha watu wangu na kwenda mbali nao, kwa kuwa wote ni wazinzi, kundi la watu wasio waaminifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Laiti ningekuwa na nyumba ya kukaa wasafiri jangwani, ningewaacha watu wangu na kwenda mbali nao, kwa kuwa wote ni wazinzi, kundi la watu wadanganyifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani, kibanda cha wasafiri; nipate kuwaacha watu wangu, na kuondoka kwao! Maana wao ni wazinzi, wote pia, mkutano wa watu wenye hiana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani, ambamo ningewaacha watu wangu na kwenda zangu.” Mwenyezi-Mungu asema: “Wote ni watu wazinzi, ni genge la watu wahaini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nataka sana, ningepata nyikani fikio la wasafiri, ningewaacha wao walio ukoo wangu na kutoka kwao, kwani wao wote ndio wagoni, ni chama cha wadanganyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani, kibanda cha wasafiri; nipate kuwaacha watu wangu, na kuondoka kwao! Maana wao ni wazinzi, wote pia, mkutano wa watu wenye hiana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ndimi zao ni hatari kama pinde; wameimarika kwa ajili ya uongo na si kwa ajili ya haki. Wanaendelea kutenda uovu kisha uovu, wala hawanitambui mimi. –Ni ujumbe wa Yawe.–