Jeremiah 9:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndimi zao ni kama mishale yenye sumu, daima haziishi kudanganya; kila mmoja huongea vema na jirani yake, lakini moyoni mwake hupanga kumshambulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndimi zao ni mshale wenye sumu, hunena kwa udanganyifu. Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake, lakini moyoni mwake humtegea mtego.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ulimi wao ni mshale ufishao; husema maneno ya hadaa; mtu mmoja husema maneno ya amani na mwenzake kwa kinywa chake, lakini moyoni mwake humwotea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndimi zao ni kama mishale yenye sumu, daima haziishi kudanganya; kila mmoja huongea vema na jirani yake, lakini moyoni mwake hupanga kumshambulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndimi zao ni mshale wenye sumu, hunena kwa udanganyifu. Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake, lakini moyoni mwake humtegea mtego.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndimi zao ni mshale wenye sumu, hunena kwa udanganyifu. Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake, lakini moyoni mwake humtegea mtego.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ulimi wao ni mshale ufishao; husema maneno ya hadaa; mtu mmoja husema maneno ya amani na mwenzake kwa kinywa chake, lakini moyoni mwake humwotea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndimi zao ni kama mishale yenye sumu, daima haziishi kudanganya; kila mmoja huongea vema na jirani yake, lakini moyoni mwake hupanga kumshambulia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndimi zao ni mishale ya kuchoma na kuua, husema madanganyifu: kwa vinywa vyao husema matengemano na wenzao, lakini mioyoni huviziana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ulimi wao ni mshale ufishao; husema maneno ya hadaa; mtu mmoja husema maneno ya amani na mwenzake kwa kinywa chake, lakini moyoni mwake humwotea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nisiwaazibu kwa sababu ya mambo haya? –Ni ujumbe wa Yawe.– Nisililipize kisasi taifa kama hili?