Job 1:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo naye kabla hajamaliza kusema, mwingine akawasili, akasema, “Wakaldayo walijipanga makundi matatu wakashambulia ngamia, wakawachukua, na kuwaua watumishi wako kwa upanga! Mimi peke yangu nimenusurika ili kuja kukuarifu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wakaldayo waliunda vikosi vitatu vya uvamizi na kuwaangukia ngamia wako na kuwachukua wakaondoka nao. Wakawaua watumishi kwa upanga, mimi peke yangu ndiye niliyenusurika kukuletea habari.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo naye kabla hajamaliza kusema, mwingine akawasili, akasema, “Wakaldayo walijipanga makundi matatu wakashambulia ngamia, wakawachukua, na kuwaua watumishi wako kwa upanga! Mimi peke yangu nimenusurika ili kuja kukuarifu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wakaldayo waliunda vikosi vitatu vya uvamizi na kuwaangukia ngamia wako na kuwachukua wakaondoka nao. Wakawaua watumishi kwa upanga, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wakaldayo waliunda vikosi vitatu vya uvamizi na kuwaangukia ngamia wako na kuwachukua wakaondoka nao. Wakawaua watumishi kwa upanga, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo naye kabla hajamaliza kusema, mwingine akawasili, akasema, “Wakaldayo walijipanga makundi matatu wakashambulia ngamia, wakawachukua, na kuwaua watumishi wako kwa upanga! Mimi peke yangu nimenusurika ili kuja kukuarifu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyu angali akisema, akaja mwingine, akasema: Wakasidi wamekuja vikosi vitatu, wakatushambulia, wakawakamata ngamia, wakawachukua, nao vijana wakawapiga kwa ukali wa panga zao, mimi nikapona peke yangu tu, nikupashe habari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule naye alipokuwa hajamaliza kusema, mwingine akafika, akasema: “Wakaldea walijipanga makundi matatu, wakashambulia ngamia, wakawatwaa, na wakaua watumishi wako kwa upanga! Ni mimi tu peke yangu nimepona kwa kuja kukuletea habari.”