Job 1:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
alikuwa na kondoo 7,000, ngamia 3,000, jozi 500 za ng'ombe na punda majike 500; na watumishi wengi sana; yeye alikuwa mashuhuri kuliko watu wote huko mashariki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye alikuwa na kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, jozi mia tano za maksai, na punda mia tano, tena alikuwa na idadi kubwa ya watumishi. Alikuwa mtu maarufu sana miongoni mwa watu wa Mashariki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
alikuwa na kondoo 7,000, ngamia 3,000, jozi 500 za ng'ombe na punda majike 500; na watumishi wengi sana; yeye alikuwa mashuhuri kuliko watu wote huko mashariki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye alikuwa na kondoo 7,000, ngamia 3,000, jozi 500 za maksai, punda 500, tena alikuwa na idadi kubwa ya watumishi. Alikuwa mtu mkuu sana miongoni mwa watu wa Mashariki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye alikuwa na kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, jozi mia tano za maksai, na punda mia tano, tena alikuwa na idadi kubwa ya watumishi. Alikuwa mtu mkuu sana miongoni mwa watu wa Mashariki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mali yake nayo ilikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watumishi wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
alikuwa na kondoo 7,000, ngamia 3,000, jozi 500 za ng'ombe na punda majike 500; na watumishi wengi sana; yeye alikuwa mashuhuri kuliko watu wote huko mashariki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Makundi yake yalikuwa mbuzi na kondoo pamoja 7000 na ngamia 3000 na majozi ya ng'ombe 500 na punda majike 500, hata watumwa wake wakawa wengi sana. Kwa hiyo yule mtu alikuwa mkuu kuliko watu wote waliokaa upande wa maawioni kwa jua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng’ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alikuwa na mali, kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, ngombe elfu moja, punda dike mia tano, na watumishi wengi sana. Yeye alikuwa wa heshima kuliko watu wote kule upande wa mashariki.