Job 2:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yobu akamjibu mkewe, “Wewe unaongea kama wanawake wapumbavu. Tukipokea mema kutoka kwa Mungu, kwa nini tukatae kupokea pia mabaya kutoka kwake?” Katika mambo hayo yote, Yobu hakutamka neno lolote la kumkosea Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamjibu, “Unazungumza kama mwanamke mpumbavu. Je, tupokee mema kutoka kwa Mungu, bali tusipokee mabaya?” Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi katika kusema kwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yobu akamjibu mkewe, “Wewe unaongea kama wanawake wapumbavu. Tukipokea mema kutoka kwa Mungu, kwa nini tukatae kupokea pia mabaya kutoka kwake?” Katika mambo hayo yote, Yobu hakutamka neno lolote la kumkosea Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamjibu, “Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavu ye yote angelinena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?” Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi kwa kusema kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamjibu, “Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavu yeyote angenena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?” Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi katika kusema kwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yobu akamjibu mkewe, “Wewe unaongea kama wanawake wapumbavu. Tukipokea mema kutoka kwa Mungu, kwa nini tukatae kupokea pia mabaya kutoka kwake?” Katika mambo hayo yote, Yobu hakutamka neno lolote la kumkosea Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamwambia: Unasema, kama wanawake wapumbavu wanavyosema; mema tuliyapokea mikononi mwa Mungu, sasa hiki kibaya tusikipokee? Katika mambo hayo yote Iyobu hakukosa kwa midomo yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akamujibu: “Wewe unasema kama wanawake wapumbafu. Tukipokea mazuri kutoka kwa Mungu, kwa nini tukatae kupokea vilevile mabaya kutoka kwake?” Katika mambo hayo yote, Yobu hakusema neno lolote la kumukosea Mungu.